Mwenyekiti
wa CCM aliemaliza mda wake Othman Gora ametetea kiti chake baada ya
kuwabwaga wagombea wenzake kwa kura 676 sawa na asililimia 76 ya kura
zote 1092 zilizopigwa katika uchaguzi ambao siku mbili kabla ya uchaguzi
huo viongozi walionekana wakitoa rushwa za wazi kwa wajumbe
ilikujipanga na uchaguzi mkuu 2020
Makundi
ya uchaguzi huo ambao wajumbe walianza minong'ono kabla msimamizi wa
uchaguzi huo hajatangaza matokeo, wapambe walianza kumtangaza mgombea
Gora kuwa ameshinda bila kujali kanuni za uchaguzi ambapo hapo kabla ya
kufika ukumbini wajumbe walionekana wakikaa vikundi na kupewa fedha
kiasi cha Elfu kumi na kupewa maelekezo ya nani anaetakiwa.
Wajumbe
1092 zaidi ya asilimia 98.99 ambao walishiriki kupiga kura, ambapo
wagombea kwa nafasi mbali mbali walikuwa nafasi ya mwenyekiti wakiwa 3
nafasi ya ujumbe wa mkutano mkuu taifa wakiwa 9 na wajumbe halmashauri
kuu wilaya wakiwa 6 na wajumbe nafasi ya uwt wilaya 7 nafasi ya wajumbe
kutoka kundi la vijana wakiwa 7.
Akisoma
matokeo hayo majira ya saa 7.15 usiku Msimamizi wa uchaguzi huo Mbunge
wa Mtera na mjumbe wa halmashauri kuu taifa Job Lusinde alimtangaza
Othman Gora kuwa mshindi wa kiti cha uwenyekiti wa wilaya hiyo kwa
kuwabwa wenzake Kimolo Iddy na Juma Fataki.
Lusinde
alisema kuwa uchaguzi huo ambao ulienda kwa uwazi na kuwapata viongozi
hao ambao wataongoza kwa kipindi cha miaka mitano na kuwataka wale ambao
kura hazikutosha wajipange kwa uchaguzi ujao na kuwa kitu kimoja katika
kukijenga chama hicho.
Akizungumza
mara baada ya kutangazwa Othman Gora alisema kuwa ushindi aliopata ni
wanaccm wote na kuahidi kushirikiana nao katika kuhakikisha chama hicho
kinaendelea kuimarika na kushinda chaguzi mbali mbali ikiwemo kuibua
miradi ya maendeleo na kuisimamia serikali.
Kwa
upande mwingine wajumbe wameulalamikia uchaguzi huo uliogubikwa na
matukio ya rushwa za wazi wazi zikiongwa na naibu waziri wa fedha
dakta.Ashatu Kijaji kwa upangaji wa safu yake kwa ajili ya uchaguzi mkuu
wa mwaka 2020 hali iliyopelekea wajumbe kupewa fedha wakitumia Makati
wa ccm wa Kata na baadhi ya madiwani.
Hata
hivyo baadhi ya wagombea wamekuwa wakiendelea na vikao vya chini kwa
chini lengo likiwa ni kukata rufaa kwani uchaguzi huo kanuni na sheria
zilikiukwa kwa kutangaza matokeo kabla ya msimamizi hajatangaza hali
katika mkutano huo ambao uliendeshwa kwa uwazi lakini ukiwa na kasoro za
upangaji wa matoke.
Pamoja
na kuwepo taasisi ya kupambana na rushwa TAKUKURU na kupewa taarifa za
wazi bado hatua hazikuchukuliwa kwa wakati lakini mwanahabari hii juzi
usiku katika kata ya Soera alishuhudia wajumbe wakipewa fedha na bwana
aliefahamika kwa jina moja Ridhiwan.
Aidha
pia huko kwenye kata za Bumbuta,Kisese,Kikore wajumbe walipewa mlungula
wa wazi ambapo Naibu waziri alidai ametumwa na makamu wa Rais na
mwenyekiti wa vijana kata ya Bumbuta Hemed alitishiwa kutolewa dirishani
kwani ameonekana kumpinga Dkta Kijaji katika malengo yake.