Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden Madembo akiwa nambunge
wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta
Kabati wakati wa kuzitambua changamoto zinazoikabili shule ya msingi
Igeleke iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Eden Madembo akiwa nambunge
wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta
Kabati wakiwa katika picha nawanafunzi wa darasa la saba
Mbunge
wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta
Kabati akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua madarasa ambayo
miundombinu yake imeharibika.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mwenyekiti
wa serikali ya mtaa wa Kihesa Kilolo B kupitia chama cha demokrasia na
maendeleo (CHADEMA) Eden Madembo amempigia magoti mbunge wa viti maalumu
mkoa wa Iringa Ritta Kabati kuwasaidia kukarabati shule ya msingi
Igeleke kwa kuwa miundo mbinu yake imeharibika na sio rafiki kwa
wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo.
Akizungumza
na blog bwana Madembo alisema shule hiyo inamiundombinu mibovu hivyo ni
hatarishi kwa wanafunzi wa shule hii kwanza toka mwaka 1978 hadi leo
shule hiyo haijawahi kufanyiwa ukarabati wa kueleweka hivyo inahitajika
kukarabatiwa haraka iwezekanavyo.
“Mwandishi
ukiangalia majengo ya shule hii unaona jinsi gani yalivyoaribika na ipo
katika halmashauri ya manispaa ya Iringa lakini viongozi wengi
hawaingalii kwa jicho la tatu kitu kinachotupa shida sisi viongozi wa
eneo hili” alisema Madembo
Madembo
alisema kuwa shule nyingi zilizojengwa miaka ya 1978 na kuendelea
zinamiundombinu ilichoka hivyo serikali na viongozi wa kisiasa kuanza
kuzitafutia mikakati ya kuzikarabati ili kuboresha taaluma kwa watoto
wetu kuendana na karne ya sasa.
“Hebu
angalia hapo juu hili paa muda wowote kuanzia sasa hili paa la darasa
linaweza kuleta maafa kwa wanafunzi lakini viongozi wetu hawaliangalii
hili swala ndio maana nimemuaomba huyu mbunge Ritta Kabati kusaidia
kuarabati” alisema Madembo
Aidha
Madembo alisema kuwa haangalii itikadika ya vyama bali anatafuta
viongozi waliotayari kule maendeleo kwa kuwa hiyo ndio tija ya kuwa
kiongozi kuwatumika wananchi waliotuchagua wakati tukiomba kura za kuwa
viongozi.
“Leo
hii mimi ni mwenyekiti wa CHADEMA lakini nipo na mbunge wa CCM
aliyekubali kuja kusaidia kuleta maendeleo katika shule yetu yaIgeleke hivyo nipende kuweka wazi kuwa mimi kwenye maendeleo siangalii chama gani kinaleta maendeleo” alisema Madembo
Kwa
upande wake mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha
mapinduzi (CCM) Ritta Kabati alisema kuwa anafanyakazi na wenyeviti wote
wa manispaa ya Iringa kwa lengo la kuijenga manispaa na kuinua uchumi
wa wananchi wa mkoa wa Iringa.
“Nimekuwa
navikao vya mara kwa mara kwa wenyeviti wa mitaa ya hapa manispaa hivyo
wenyeviti wa CHADEMA wamekuwa wa kwanza kuniita kila wakati kusaidia
kuleta maendeleo katika maeneo husika ndio maana leo unaniona nipo na
mwenyekiti wa CHADEMA kutafuta njia mbadala ya kutatua changamoto za hii
shule ya Igeleke” alisema Kabati
Kabati aliwataka viongozi mbalimbali kutafuta njia mbadala ya kuwaletea maendeleo wananchi nsio kuangalia vyama vinafanya nini.
“Mimi
ni kada wa chama cha mapinduzi lakini nimekuwa nikifanya kazi vizuri na
viongozi mbalimbali wa kiasa kwa lengo la kuleta maendeleo tu ndio
sababu inayosababishwa wapinzani kuniona mimi bora wakati wa kufanya
shughuri za kuleta maendeleo” alisema Kabati
Kabati alisema kuwa ataendelea kufanya ziara kwenye shule zote zenye matatizo ili kuzisaidia kuyatatua matatizo hayo na leo amefanya ziara katika shule ya msingi Igeleke kwa kuziona changamoto zinazoikabili shule hiyo ili kuzitafutia ufumbuzi.
Naye
mkuu wa shule ya msingi Igeleke Robert Mulilo na mwenyekiti wa kamati
ya shule hiyo Wakati Maliva walimshukuru mbunge Ritta Kabati kwa
jitihada zake za kuendelea kuboresha miundombinu ya shule za msingi
katika halmashauri ya manispaa ya Iringa.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia