Ticker

6/recent/ticker-posts

MVUA YAUWA MUUGUZI WA HOSPITAL YA ST ELIZABETH

Aliyesimama mbele ya jengo la hospital ya st  Elizabeth hahusiani na tukio






Mvua iliyokuwa ikinyesha Alfajiri ya Leo May 16,Mwaka huu imesababisha kifo cha muuguzi Mmoja Wa kike Wa hospital ya Wilaya ya St Elizabeth ambaye amesombwa na mafuriko wakati akielekea kazini kwake.
Kwa mujibu Wa mganga Mkuu Wa hospital hiyo Dkt Joslin Mlay amemtaja marehemu kuwa ni Alodia Silvesta anayekadiliwa kuwa na umri Wa miaka 60
Amesema muuguzi huyo amekumbwa na masahibu hayo umbali wa Mita mia moja kabla ya kufika hospitalini hapo  majira ya SAA 15 Asubuhi katika ukuta wa kanisa la Lutheran uliopakana na hospital hiyo ya st Elizabeth.
'Marehemu alikuwa akivuka kidaraja kidogo ndipo alipoteleza na kusomba na maji ya mvua umbali Wa Mita 100 ambapo kikosi cha zima moto na wokozi waliweza kutoa mwili uliokuwa umekwama kwenye Kara Vatican edema Dkt Mlay
Mwili Wa marehemu umepelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospital ya rufaa ya Mount Meru Mkoa Wa Arusha

Post a Comment

0 Comments