Uzinduzi huo umefanyika leo Jumatano Mei 16,2018 katika ukumbi wa Lewis Kalinjuna uliopo katika ofisi za Manispaa ya Shinyanga. Mkuu
huyo wa wilaya amekabidhi vitambulisho 12,918 kwa maafisa watendaji wa
kata 17 za manispaa hiyo watakaokwenda kugawa vitambulisho hivyo kwa
wananchi.
“Hapa
nchini, hili ni zoezi la kwanza la ugawaji vitambulisho kwa wananchi kwa
kutumia ugawaji wa mkupuo,tunaanzia katika manispaa ya
Shinyanga,nakabidhi rasmi vitambulisho hivi kwa maafisa watendaji wa
kata ambao watagawa vitambulisho kwa wananchi”,alieleza Matiro.
Aidha
aliwataka maafisa watendaji kuwa makini na kugawa vitambulisho hivyo
haraka huku akisisitiza kuwa vitambulisho hivyo havitolewi kwa ubaguzi
bali kila mwananchi ana haki ya kupata.
“Zoezi
kujiandikisha linaendelea katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga
lakini kwa upande wa manispaa ya Shinyanga tumemaliza zoezi la
uandikishaji kinachoendelea sasa ni kugawa vitambulisho,hili ni zoezi
endelevu wale ambao hawajiandikisha wafike katika ofisi za NIDA
kujiandikisha ili wapate vitambulisho”,aliongeza Matiro.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo,Mratibu wa NIDA mkoa wa Shinyanga Nathanael
Fredrick Njau alisema tangu waanze zoezi la uandikishaji mwezi Septemba
2017 katika manispaa ya Shinyanga wamezalisha jumla ya vitambulisho
17,780 na tayari wameshagawa vitambulisho 3651 kwa watumishi wa umma na
leo vitambulisho 12,918 kwa wananchi na zoezi la uandikishaji na ugawaji
vitambulisho linaendelea.
Naye
Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Vihatarishi NIDA Makao makuu,Stephen
Kapesa aliwasisitiza wananchi ambao bado hawajisajili waendelee
kujisajili katika ofisi za Uhamiaji huku akiwataka kutoa ushirikiano
kuwafichua watu wasiostahili kupata vitambulisho hivyo.
“Uzalishaji
wa vitambulisho unaendelea na tunatarajia hadi mwezi Desemba mwaka huu
kila mwanachi awe na kitambulisho,NIDA inaomba wananchi kufichua watu
wasiotahili kupata vitambulisho hivi wakiwemo wahamiaji
haramu”,aliongeza Kapesa.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Geofrey
Mwangulumbi aliwataka maafisa watendaji kutoendekeza urasimu katika
ugawaji wa vitambulisho na hatarajii kusikia kitambulisho cha mwananchi
kimepotea. 
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza wakati wa
uzinduzi rasmi wa zoezi la kugawa vitambulisho vya taifa (NIDA) kwa
wananchi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga. Kushoto ni Naibu
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Agnes Machiya. Kulia ni Mkuu wa
Kitengo cha Usimamizi wa Vihatarishi NIDA Makao makuu,Stephen Kapesa -
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza wakati wa
uzinduzi rasmi wa zoezi la kugawa vitambulisho vya taifa (NIDA) kwa
wananchi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akiwasisitiza maafisa
watendaji wa kata kuwa makini katika zoezi la ugawaji vitambulisho kwa
wananchi ili kuepuka changamoto inayoweza kujitokeza ya kupotea kwa
vitambulisho.
Mratibu
wa NIDA mkoa wa Shinyanga Nathanael Fredrick Njau akisoma taarifa ya
zoezi la uandikishaji na utoaji vitambulisho vya taifa katika Manispaa
ya Shinyanga.
Mkuu
wa Kitengo cha Usimamizi wa Vihatarishi NIDA Makao makuu,Stephen Kapesa
akizungumzia kuhusu zoezi la utoaji vitambulisho vya taifa.
Maafisa watendaji,madiwani na watumishi mbalimbali wa manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi akizungumza
wakati wa uzinduzi wa zoezi la ugawaji vitambulisho.
Naibu
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Agnes Machiya akimkaribisha mkuu
wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro kuzindua rasmi zoezi la ugawaji
wa vitambulisho vya taifa kwa wananchi wa manispaa ya Shinyanga.
Sehemu
ya vitambulisho 12,918 vilivyokabidhiwa kwa maafisa watendaji wa kata
17 za manispaa ya Shinyanga watakaokwenda kugawa vitambulisho hivyo kwa
wananchi.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akimkabidhi
Kitambulisho cha taifa Naibu Meya wa Manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya
wakati akizindua rasmi zoezi la kugawa vitambulisho vya taifa (NIDA)
kwa wananchi wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
Mkurugenzi
wa halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi akionesha
kitambulisho chake cha taifa baada ya kukabidhiwa na mkuu wa wilaya ya
Shinyanga Josephine Matiro.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akimkabidhi
Kitambulisho cha taifa diwani wa kata ya Lubaga Mchungaji Obedi Jilala
(CHADEMA).
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akimkabidhi
Kitambulisho cha taifa diwani wa viti Maalum Manispaa ya Shinyanga
Mariam Nyangaka (CCM).
Diwani wa kata ya Kizumbi,Reuben Kitinya akipokea kitambulisho cha taifa.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akikabidhi
Vitambulisho vya taifa kwa afisa mtendaji wa kata ya Mwawaza,Nhiga Nhiga
ili akavigawe kwa wananchi.
Mkuu
wa wilaya ya Shinyanga mheshimiwa Josephine Matiro akikabidhi
Vitambulisho vya taifa kwa afisa mtendaji wa kata ya Ndembezi,Felister
Msemelwa ili akavigawe kwa wananchi wa kata hiyo.
Mratibu
wa NIDA mkoa wa Shinyanga Nathanael Fredrick Njau akisisitiza jambo
wakati wa zoezi la ugawaji vitambulisho vya taifa kwa maafisa watendaji
wa kata za manispaa ya Shinyanga.