Ticker

6/recent/ticker-posts

BENKI YA CRDB KUFANYA MKUTANO WA WANAHISA JIJINI ARUSHA

IMG_5511

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt.Charles Kimei akizungumza na vyombo vya habari jijini Arusha leo ,kuhusu mkutano mkuu wa ishirini na tatu wa Wanahisa unaotarajia kuanza rasmi tatehe 18 na 19 utakaohudhuriwa na wanahisa zaidi ya Elfu moja  katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC uliopo jijini Arusha(Habari Picha na Pamela Mollel,Arusha)
IMG_5506
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt.Charles Kimei kushoto,kulia ni Mkurugenzi wa mikopo James Mabula  kulia 
IMG_5504
Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa masoko wa CRDB Jadi Ngwale,kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt.Charles Kimei
IMG_5510
Waandishi wa habari wakiwa wanafanya mahojiano ya kina kuhusu mkutano huo 

Na Pamela Mollel,Arusha

Benki ya CRDB inatarajia kufanya mkutano wake wa ishirini na tatu(23)wa wanahisa wa benki hiyo katika ukumbi wa Kimataifa wa AICC ulipo jijini Arusha na kuhudhuriwa na watu zaidi ya Elfu moja.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Dkt.Charles Kimei alisema kuwa mkutano huo wa wanahisa unatarajiwa kufanyika tarehe 19 mwezi huu

Dkt.Kimei alisema kuwa Mkutano huo wa wanahisa wa benki ya CRDB utatanguliwa na semina maalumu kwa wanahisa wa benki hiyo utakaofanyika tarehe 18 mwenzi huu ambapo pamoja na mambo mengine wanahisa watapata fursa ya kufahamu mambo mbalimbali kibenki

Alisema kuwa agenda za mkutano huo ni kupokea na kupitisha taarifa za fedha na ripoti za wakurugenzi kwa mwaka uliopita tarehe 31 mwezi Disemba 2017,kuhidhinisha taarifa maalumu ya gawiyo wa mwaka ,kuchagua wajumbe wa bodi ,kuhidhinisha uchaguzi wa wakaguzi wa hesabu wanaokupalika kisheria

Dkt Kimei alitoa rai kwa wanahisa wa benki hiyo kuuhudhuria kwa wingi katika mkutano huo mkuu huku akiongeza kuwa kwa mwanahisa ambaye hataweza kuudhuria anahaki ya kuchagua mwakilishi au wawakilishi kuudhuria na kupiga kura kwa niaba yake

Post a Comment

0 Comments