
Afisa Afya halmashauri ya Arusha, Issa Msumari
akiongea katika
Mafunzo siku moja ya ujazaji wa takwimu za uwepo wa vyoo bora katika maeneo yao mafunzo yaliyoshirikisha
Maafisa Watendaji wa kata 14 na maafisa watendaji wa vijiji ndani ya kata
.
Halmashauri ya Arusha kwa kushirikiana na shirika lisilo la Maendeleo la SNV la nchini Uholanzi wametoa mafunzo kwa watendaji a kata 14 juu ya ujazaji wa takwimu za uwepo wa vyoo bora katika maeneo yao.
Halmashauri ya Arusha kwa kushirikiana na shirika lisilo la Maendeleo la SNV la nchini Uholanzi wametoa mafunzo kwa watendaji a kata 14 juu ya ujazaji wa takwimu za uwepo wa vyoo bora katika maeneo yao.
Mafunzo hayo ya siku moja yamehusisha Maafisa Watendaji wa kata 14 na
maafisa watendaji wa vijiji ndani ya kata hizo, ili waweze kufuatilia
takwimu za aina za vyoo, vinavyotumika kwenye kaya kwa kulinganisha na
aina ya nyumba ya kaya husika.
Akizingumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Afisa Afya
halmashauri ya Arusha, Issa Msumari, amesema kuwa, watendaji wa kata na
vijiji wanatakiwa kupita nyumba kwa nyumba, kufanya ukaguzi wa vyoo
vinavyotumika kwenye kaya na kutambua aina ya vyoo kwa kulinganisha na
nyumba inayotumika.
Ameongeza kuwa, takwimu hizo zitasaidia kutambua hali halisi ya
matumizi ya vyoo bora katika maeneno hayo, kufuatia mafunzo ya
uhamasishaji ya ujenzi wa vyoo bora yaliyotolewa kwenye kaya hizo
kufuatia kampeni ya nyumba ni choo.
"Imeonekana kuwa, kaya inajenga nyumba bora ya kuishi na kusahau
ujenzi wa choo bora, bila kufahamu kuwa nyumba ni choo, unakuta nyumba
nzuri but choo cha ovyo,hakina hata usiri, kimezungushiwa maturubai".
amesema Msumari
Hata hivyo Afisa Afya huyo, amefafanua kuwa, takwimu zinaonesha kuwa
asilimia 3 ya wakazi wa halmashauri ya Arusha hawana vyoo bora na
kuongeza kuwa kupitia kampeni ya nyumba ni choo, halmashauri inategemea
kufikia aslimia 100 ya matumizi ya vyoo bora mwishoni mwa mwaka huu.
Mshauri wa masula ya Usafi na Mazingira wa shirika la SNV, Anna
Emmanuel, amesema kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kuhakikisha watendaji
wanakusanya takwimu sahihi za matumizi ya vyoo, kwenye kaya katika
maeneo yao.
Takwimu hizi zitatoa taswira ya hali halisi ya matumizi ya vyoo,
ambazo zitawezesha kupata hali halisi ya mabadiliko ya tabia ya jamii
kutoka kwenye tabia ya kunya nje na kwenda kunya chooni, kwa kuwa tendo
hilo ni la siri na linahitaji choo bora.
Naye Afisa Mtendaji wa kijiji cha Oljoro, Lootha Sikoreim
amethibitisha kuwa, watu wengi katika maeneo ya vijijini, wanapojenga
nyumba, choo huwa hakipo kwenye bajeti, mara nyingi hujenga kwa hutumia
vifaa vilivyobaki baada ya ujenzi wa nyumba kukamilika.
"Ni kawaida mtu anajenga nyumba, baada ya nyumba kukamilika anatumia
vipande vya tofali, mabaki ya mabati, saruji kujenga choo, kwa hali hiyo
lazima choo hakitalingana na nyumba, na wakati mwingine pesa ikiisha
basi choo hakitajengwa" amesema Sikorei
Hata hivyo elimu inaendelea kutolewa kwa wananchi, ili kuhakikisha
ujenzi wa nyumba unaendana na ujenzi wa vyoo ili kuwe na uwiano kati ya
nyumba na choo.
Maafisa Watendaji waliopata mafunzo hayo ni wa kata za Nduruma,
Lemanyata, Bwawani, Musa, Laroi, Oldonyosambu,Kisongo, Oldonyowas,
Tarakwa, Sambasha, Oljoro, Kiutu na Olturoto.