
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameionya Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA) kuacha kutumia lugha zenye kuudhi wananchi pindi
wanapokwenda kukusanya kodi kwa wafanyabiashara katika maeneo yao ya
kazi pamoja na kutowatoza kodi kubwa ambayo haina uhalisia.
Waziri Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Mei 03, 2018 Bungeni
Jijini Dodoma kwenye kikao cha 21 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la Mbunge rank Mwakajoka
aliyetaka kujua Serikali inatoa kauli gani kuhusu matatizo
wanayofanyiwa wafanyabishara na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
"Wafanyabiashara wote kwanza wawe na amani katika
kufanyabiashara zao nchini na wawekezaji wote waendelee kuwekeza na
kuongeza mtaji zaidi ili kuekeza zaidi kwa sababu serikali imedhamiria
kufungua milango ya uwekezaji nchini. Tunajua kwamba kodi ni wajibu wa
kila mmoja kadiri ya shughuli zake zinazomletea mapato ilivyo kwa ukubwa
wake. Kwa hiyo tumeielekeza TRA ihakikishe inapokwenda kukusanya kodi
haitumii lugha ya kuudhi wala nguvu", amesema Majaliwa.
Pamoja na hayo, Majaliwa ameendelea kwa kusema "ndio maana
tulianzisha kitengo cha elimu ndani ya TRA ikiwa na lengo la
kumuelimisha mwananchi umuhimu wa kulipa kodi, hakuna sababu ya
kumlazimisha mlipa kodi. Pale patapotokea malalamiko wafanyabiashara
wana uhuru mkubwa wakuenda kwa kiongozi mkubwa wa eneo hilo ili
kulalamikia jambo hilo ili sheria zipate kuchukuliwa".
Kwa upande mwingine, Waziri Majaliwa amesema serikali haina
ugomvi na wafanyabishara na TRA wanapaswa kufanya kazi vyema huku
akiwaomba wafanyabiashara kutoa taarifa pindi wanapobughudhiwa na TRA
wasiwapandishie, kodi wafanyabiashara.