Na Woinde Shizza,Arusha.
Meya wa Jiji
la Arusha Kalisti Lazaro amependekeza kuundwa kwa baraza la Wanaume ambalo
litasaidia kuhamasisha uwajibikaji wa wanaume kuanzia ngazi ya familia,jamii na
taifa hivyo kuchochea maendeleo kwa ujumla.
Kalisti
akizungumza katika Mahafali ya darasa la Wanaume lilioandaliwa na taasisi
ya wanaume ya Men At Work yenye makao
yake jijini Arusha,alisema kuwa mafunzo maalumu kwa wanaume yatasaidia
kupunguza wimbi la wanaume wengi kutelekeza familia na watoto pamoja na
kuimarisha familia bora ambazo zitajenga taifa bora.
Alisema kuwa
migogoro mingi inatokea kwenye familia nyingi kwa sababu ya wanaume
wasiojielewa hivyo wanaume wakijitambua na kusimama kwenye nafasi zao familia
zitapona na taifa litapona.
“kuna
changamoto Sera za nchi haziongelei wanaume,sera zinawaongelea wanawake,vijana
wa kike na wa kiume wanazungumziwa hata katika mikopo lakini wanaume
hawajaongelewa kwenye sera” Alisema Meya
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Men At Work Maxwell Stanslaus amesema kuwa mafunzo ya wanaume
yanaongeza thamani ya wanaume ,wanaume wakijitambua na kujiboresha wanakuwa bora zaidi.
Baadhi ya
Wahitimu wa darasa la Wanaume Christopher Kombe na Emanuel Vicent wameeleza
kuwa darasa hilo limewasaidia kujua namna bora ya uendeshaji wa familia kwani wanaume ni msingi wa familia na taifa.