
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Will J. Njau wakati wa
ufunguzi wa mkutano wa robo ya 3 wa baraza la Halmashauri hiyo amesema
mbali na changamoto ndogo ndogo zilizopo kwenye Halmashauri hiyo
,Mwenendo wake unaridhisha kwani ukusanyaji wa mapato umefikia asilimia
68.2 kiasi ambacho ni cha juu ikizingatia kuna vyanzo kama 3
vilivyotwaliwa na Serikali kuu kikiwemo ushuru wa mabango, pia
Halmashauri hiyo imezawadiwa gari kwa kufanya vizuri kwenye Usafi na
Mazingira , pia imeshika nafasi nzuri kwenye ufaulu wa shule za
sekondari na msingi .
Baadhi ya wajumbe ambao ni madiwani wamelalamikia kitendo cha fedha
za miradi ya maendeleo kutokupelekwa jambo linalosababisha miradi mingi
kusimama kwenye Kata ambapo makamu mwenyekiti wa Halmashauri
hiyo,Nelson Mafie ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya fedha ,mipango na
utawala amewashauri wajumbe hao kujiridhisha kama miradi wanayoisemea
ipo kwenye bajeti.
Nae Kaimu mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Dkt.Amani Sanga amefafanua
kuwa kwa mwaka wa fedha 2017/2018 Halmashauri hiyo ilipitisha kwenye
bajeti yake fedha kutoka mapato yake ya ndani kiasi cha Biliono
2,226,374,000 kwa ajili ya miradi ya maendeleo hadi sasa zaidi ya
milioni 350,270,430 ya fedha hizo imepelekwa kwenye miradi ya maendeleo
,pia amesema fedha zinazopelekwa kwenye miradi ya maendeleo hutegemea
ukusanyaji wa mapato.
Aidha mkutano huo wa baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Meru ambao ni
wa siku 2 umehairishwa kwa siku ya kwanza ukiwa na azimio kuwa
halitapokea taarifa za utekelezaji wa kata ambazohazija fuata utaratibu
wa kisheria wa kujadiliwa na kupitishwa kwenye baraza la maendeleo ya
Kata (WDC) .