
Kutokea Mahakamani Kisutu ni kwamba mrembo Wema Sepetu ameshindwa
kujitetea katika kesi yake ya kutumia dawa za kulevya baada ya kuugua
ghafla akiwa mahakamani hapo.
Wakili wa Serikali, Costanine Kalula amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu,
Thomas Simba kuwa shauri hilo limeitishwa ili Wema na wenzake waanze
kujitetea, lakini Wema anaumwa, hivyo anaomba kesi iahirishwe hadi
tarehe nyingine.
Baada ya kueleza hayo, Mama mzazi wa Wema Sepetu, Miriam Sepetu
aliieleza mahakama kuwa Wema alifika mahakamani hapo lakini wakati
anasubiri kuingia mahakamani alianza kuumwa ambapo alianza kutapika na
hivyo kuondoka.
Baada ya maelezo hayo , Hakimu, Thomas Simba ameahirisha kesi hiyo hadi
May 29 na 30, 2018 ili washtakiwa watakapoanza kujitetea.
Mbali na Wema, washtakiwa wengine ni Angelina Msigwa na Matrida Abbas.
Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka mawili ya kukutwa na kiwango kidogo cha dawa za kulevya na kuzitumia.
Inadaiwa February 4, 2017 katika makazi ya Wema eneo la Kunduchi Ununio,
washtakiwa walikutwa na msokoto mmoja na vipisi vya bangi vyenye uzito
wa gramu 1.08.
Kwa upande wa Wema yeye anadaiwa kuwa February mosi 2017 katika eneo
lisilojulikana jijini Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya
bangi