
Mwandishi wa habari wa kujitegemea jijini Arusha, Lucas Muyovera
amenusurika kuuawa kwa kipigo baada ya kutekwa na watu wasiojulikana
usiku wa kuamkia leo Jumatatu Mei 14,2018.
Mwanahabari huyo ambaye kwa sasa amelazwa katika hospitali ya Mkoa Mount
Meru akipatiwa matibabu inaelezwa hali yake ni mbaya baada ya watu hao
wapatao watano kumteka Jana majira ya saa tatu usiku katika eneo la
Ngulelo jijini Arusha.
Kwa mujibu wa Mwandishi huyo watu walimpakia kwenye gari yao na baadaye
kumpeleka katika mto ambao hajaufahamu na kuanza kumshambulia wakiwa
wamemvua nguo zote na kumdhalilisha.
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Arusha Claude Gwandu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
"Ni kweli Mwandishi mwenzetu,Lucas Myovela wa kituo cha Sunrise cha
jijini hapa jana usiku alitekwa,akapigwa sana,akapigwa picha za video
akiwa uchi na kisha akalazimishwa kutoa password ya simu yake wakampora
pesa, Issue iko Polisi na watuhumiwa wamekamatwa,bado tunafuatilia kwa
karibu",amesema Gwandu.
Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha limethibitisha tukio hilo likidai bado wanafanya uchunguzi