Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas akisaini kitabu cha wageni ali[powasili katika katika
Taasisi ya Umoja wa Mataifa (UN) ya kushughulikia Masuala yaliyoachwa
na Mahakama za jinai za umoja wa mataifa zilizoko eneo la Laki laki
jijini Arusha nchini Tanzania .Kulia kwake ni Msimamizi Mkuu wa Msajili wa Mahakama Sera Attika
Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas (katikati) akiwa katikaMahakama za jinai za umoja wa mataifa zilizoko eneo la Laki laki jijini Arusha Tanzania ,kushoto ni Msimamizi Mkuu wa Msajili wa Mahakama hiyo Sera Attika.Kulia ni Afisa Mkuu wa Mambo ya nje katika taasisi hiyo Ousman Njikam (picha na Woinde Shizza, Arusha).
Msajili wa Mahakama ya jinai ya Umoja wa Mataifa UN nchini Tanzania Sera Attikaakifafanua jambo kwa Waziri wa Mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas ,katikati ni Afisa Mkuu wa Mambo ya nje katika taasisi hiyo Ousman Njikam ,kufuatia ziara ya kwanza ya Wwaziri huyo kutembeleaTaasisi
ya Umoja wa Mataifa (UN) ya kushughulikia Masuala yaliyoachwa na
Mahakama za jinai za umoja wa mataifa zilizoko eneo la Laki laki .
Na Woinde Shizza,Arusha.
Waziri wa Mambo
ya nje wa Ujerumani Heiko Maas ametembelea Ofisi za Umoja wa Mataifa ya
kushughulikia Masuala yaliyoachwa na Mahakama za jinai za umoja wa mataifa
pamoja na kujionea makavati yaliyowekwa kumbukumbu za upelelezi,mashtaka na
mwenendo wa kesi.
Waziri huyo
aliambatana na balozi za Ujerumani
nchini Tanzania alipokuwa katika ziara yake ya siku moja ambapo alipata
kujulishwa juu ya shughuli za za taasisi hiyo ambayo imejikita katika kuwasaka
watuhumiwa ambao bado hawajakamatwa ,kuwalinda waathirika na mashahidi wa
mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda.
Ziara ya
waziri huyo ni ziara ya kwanza barani Afrika tangu ateuliwe kuwa waziri march 2018 ,ziara
hiyo ni muendelezo wa Nchi ya Ujerumani ambapo amesema kuwa wanafurahi katoa mchango kwa taasisi hiyo ya kimataifa
pamoja na kuimarisha mahusiano kati ya Ujerumani na bara la Afrika.
Afisa Mkuu
wa Mambo ya nje katika taasisi hiyo Ousman
Njikam amemkaribisha Waziri huyo katika jengo la mahakama ambapo shughuli za
kimahakama zinaendeshwa ,mahakama hiyo inaendelea na kazi yake ili kutoa haki
kwa walalamikaji na walalamikiwa .
Msimamizi
Mkuu wa Msajili wa Mahakama Sera Attika amesema kuwa mahakama hiyo ina sehemu
maalumu za maabusu,na maktaba yenye makavati yaliyobeba historia ya Mauaji ya
Rwanda ambayo hutumika kwa utafiti .
Waziri huyo
ametembelea taasisi za kimaitaifa ikiwemo Mahakama ya Haki za binadamu ya
Afrika na Jumuiya ya Afrika Mashariki.