RIADHA ARUSHA YAPINGA KUFUNGIWA MBIO ZA JOHN ANKWARIWoinde Shizza ,Arusha

Chama cha Riadha Mkoa wa Arusha kimepinga kufungiwa Mbio za Mwanariadha mkongwe John Akwari  ambazo zilipangwa kufanyika Juni 10 na kumtaka Katibu Mkuu wa Riadha Taifa Wiliam Gidabuday kutafakari upya kauli yake kwani inawanyima fursa wanariadha wanaochipukia.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya  Mbio hizo kufungiwa ,Chama hicho kimeanusha kufungiwa kwa mbio hizo na kusisitiza kuwa mbio hizo zitafanyika kwani hakuna kikao cha taifa kilichoamua kufungia mbio hizo isipokua utashi wa Katibu huyo 
 Alfred Oshahanga  Katibu wa Chama cha Riadha mkoa wa Arusha awana mgogoro wowote na  mbio hizo zipo pale pale

Wameeleza kupokea kwa masikitiko kufungiwa kwa mbio hizo jambo ambalo wanalipinga vikali na kueleza kuwa mbio hizo zinaenzi juhudi za muasisi na mwanariadha anayeheshimika kitaifa na kimataifa ambapo mbio hizo pia zitashirikisha wakimbiaji kutoka nje ya nchi hivyo kukuza utalii

 Meta Petro Mjumbe wa Kamati Tendaji Chama cha Riadha Taifa

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia