NCHIMBI AZINDUA SHEREHE ZA JANDO KWA VIJANA WA KIMASAI




WAZIRI wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Emanuel Nchimbi akivalishwa shuka la kimasai kwa ajili ya kupewa shukurani ya kwenda kwenye sherehe hizo

waigizaji wa kikundi cha sekei youth group wakiwa wanaonyesha igizo 

WAZIRI wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Emanuel Nchimbi ametaka
Watanzania kuzingatia maadili yatokanayo na Mila na desturi ikiwa ni
pamoja na kudumisha mila zao.

Waziri huyo alisema kuwa ikiwa Watanzania wataweza kudumisha mila na
desturi zao hali hiyo itasaidia kuongezeka kwa maadili hususani kwa
vijana ambao kwa hivi sasa maadili yamepungua kwa kiasi kikubwa.

Nchimbi alitoa rai hiyo jana katika kata ya Enaboishu iliyopo wilayani
Arumeru mkoani hapa wakati alipokuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa
sherehe za jando kwa vijana wa kiume wa rika la "Ilkishiru" zoezi
lililoanza jana.

Alisema kuwa hapa nchini makabila mengi yamepuuza mila na desturi zao
ambapo alisema kwua Wamasai wanaongoza kwa kufuata na kutunza mila
zao.

Aliyataka makabila mengine hapa nchini kuiga mfano huo wa wamasai kwa
kuendeleza tamaduni zao kwa vizazi vyao na vijavyo.



"Utamaduni huu wa kudumisha mila unatakiwa kuigwa na makabila mengine
kwani tabia ya vijana kutojali na kutokuheshimu wazazi na wakubwa hao
umekithitri hapa nchini hivyo kupitia mila na desturi hizo maadili
yaliyoporomoka yatanogezeka"alisema

Aidha aliwataka vijana kuhakikisha kuwa wanapodumsiah mila na desturi
zao kuzingatia hali ya sasa ya dunia.

Alisema kuwa hata katika zoezi hilo la jando,kuwashirikisha wataalamu
wa kisasa wa tiba.

Nchimbi aliwataka kuhakikisha kuwa wanalinda rasilimali walizonazo
ikiwa ni pamoja na kubadilika na kuweka mbinu za kisasa za kilimo na
ufugaji bora ili waweze kuondokana na hali ya umasikini.

Akisoma risala kwa niaba ya wenzake wanaokwenda jando Moikan
Mesheti,alisema kuwa kuporomoka kwa maadili kunatokana na utandawazi
uliopo hivi sasa huku vijana wengi wakikimbilia mijini kutafuta maisha
na kuacha shughuli za asili(ufugaji) maeneo ya vijijini.

Aliiomba serikali kuhakikisha kwua maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili
ya shughuli za mila na desturi kupewa hati miliki ili waweze kuhifadhi
mila na desturi.

Alisema kuwa kwa mila zao Rika hupishana kila baada ya miaka 14 ambapo
zoezi hilo hufanyika,ambapo pia waliipongeza serikali kwa kudumisah
mila na desturi.

Pia waziri huyo alijitolea kumsomesha kijana mmoja mwenye umri wa miaka saba aliyejulikana kwa jina la Edward Losanye mkazi wa Olkolada na nimwafunzi wa shule ya msingi Enguita anayesoma darasa la tano ambaye ndio kijana mdogo kuliko wate ambaye anapelekwa jando .

"mimi najitolea kumsomesha huyu mtoto kuanza hapa alipo mpaka sekondari kwakuwa ndio kina mdogo anayejiamini na ameamua kwenda jando akiwa mdogo Tanzania tunaitaji vijana wakaka mavu na majasiri kama hawa amenifurahisha sana"Alisema





Waziri wa habari vijana utamaduni na michezo Emanuel Nchimbi akiwa na mwenyeji wake naibu waziri wa aridhi nyumba maendeleo na makazi Godluck Ole Medeye wakiwa wanajadili jambo




Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post