kutoka Kulia Phidesia Mwakitalima, katibu wa Jumuiya ya wazazi ccm wilaya Arusha Rehema mohamed , Augustino
Masawe wawakilishi kamati ya utekelezaji wazazi wilaya ya Arusha wakiwa na
Afisa ustawi wa jamii jiji la Arusha Mussa mkamate katika mazungumzo juu ya Mahabusu ya watoto
Arusha.
picha ikionyesha uchakavu wa vyoo vya mahabusu ya
watoto Arusha pamoja na pakti za viroba ambavyo wanakunywa kisiri siri na kuletewa
kinyemela na vijana wa mtaani kutokana na kukosa ulinzi kwa mahabusu hayo pia
kukosekana kwa uzio katika magereza hiyo ya watoto , na imeonekana pia kuna matundu ya mapaa ya mabati ambayo ayapo pichani Matundu ambayo yamechakaa yanatumika na watoto
hao kama njia ya kutorokea nje ambapo mara kadhaa hukamatwa wakiwa wanatoroka na kurudishwa ndani
Na Woinde Shizza,Arusha
Kamati ya utekelezaji Jumuia ya
wazazi wilaya ya Arusha inatarajia kutembelea
mahabusu ya watoto Arusha katika kuazimisha sherehe ya wiki ya wazazi
Tanzania inayofanyika kila april 2 kila mwaka .
Katika maazimisho hayo pia kamati
hiyo imejipanga kukarabati baadhi ya miundo mbinu ya kituo cha mahabusu ya
watoto iliyopo jijini hapa .
Akizungumzia maadhimisho hayo katibu
wa jumuiya ya wazazi CCM wilaya ya
Arusha Rehema Mohamed alisema wao kama wazazi wamegundua kuna changamoto
nyingi katika mahabusu ya watoto mkoani Arusha ambazo wazazi kama walezi
wameona ni vyema kutembelea mahabusu ya watoto kuwaona na kuwapelekea chochote kinachopatikana .
Alisema kuwa wanajaribu pia kutatua changamoto nyingi wanazokabiliana nazo
ili kuweza kuwasaidia watoto hao nao waishi kama watoto wengine walioko
majumbani .
“kwa kweli natoa wito kwa wazazi wote
watakaoguswa Arusha kujumuika nasi tar 2 mwezi wa nne kuanzia saa 3kamili
asubuhi kwani watoto wengine wazazi wao
wamewatelekeza kabisa na wengine hawana wazazi kabisa”alisema Rehema
Kwa upande wake mjumbe wa Kamati hiyo Phidesia Mwakitalima alisema kuwa Watoto hawa wengine
wazazi wao hawaji kuwaona wengine hawana wazazi wanakabiliana na changamoto
nyingi sana ikiwemo pia kesi zao kwenda taratibu.
Mwakitalima alisema kwa sababu watoto waliopo katika mahabusu
hiyo ni watoto wenye haki ya kupata elimu hivyo pia aliomba serekali ijaribu kuwafikiria
watoto hawa ambao wapo mahabusu .
Ameongeza kuwa endapo watoto hao
watapatiwa elimu wakiwemo mahabusu
itawasaida kwani hata wakiondoka hapo hawataondoka bure na pia atatoka na elimu ambayo itamsaidia ata
akienda kuondoa ujinga mtaani na pia itamsaidia ata kutoweza kujiingiza katika
makundi mabaya ya mtaani kwani atakuwa na elimu kidogo ambayo itamsaida katika
maisha yake.
Aidha aliomba serekali pia iangalie mahabusu
hiyo kwani watoto wengine kesi zao
zinasikilizwa mda mrefu bila suluhu na makosa mengine kisheria likifikishwa
mahakamani kesi inapaswa kuisha siku hiyo hiyo
“mfano hapa kuna kesi ya mauaji
mtoto alimsaidia dada yake asichomwe kisu na shemeji yake akachukua kisu
akamuwahi shemeji yake na amekubali kosa lakini mwaka wa pili mahakamani wanasema
ushahidi haujakamilika hivyo jamani naomba serekali iangalie sana hawa watoto
kwani mbali na yote wanateseka wasaidie angalau kesi zao zisikilizwe kwa wakati
na watendewe haki jamani kiukweli inauma naomba
serekali iwaangalie awa watoto jamani “alisema Phidesia
Aidha aliomba serekali kuangalia kwa
makini sana mahabusu hii ya watoto kwani
mbali na hivi pia mahabusu hii watoto wakiumwa wanapelekwa hospital na pikipiki
hakuna gari ya mahabusu saa nyingine dawa zinakosekana na maafisa kujikuta
wakijipapasa mifukoni mwao kunusuru watoto umauti usiwakute.