Sunday, April 3, 2011
ANDENYENYE CUP KUANZA KUTIMUA VUMBI APRILI 9
Posted by woinde on Sunday, April 03, 2011 in | Comments : 0
Jeshi la polisi mkoani hapa limeandaa mashindano ya mpira wa miguu yajulikanayo kama Andengenye Cup ambayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi April 9 mwaka huu katika kiwanja cha kumbukumbu za sherkh Amri Abeid.
Akiongea na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoani hapa ambaye jina lake ndo limebeba mashindano mazima Thobias Andengenye alisema kuwa mashindano hayo yatashirikisha timu mbalimbali za mkoani hapa zikiwemo za polisi pamoja na wananchi.
Alisema kuwa jeshi la polisi limeamua kuandaa mashindano haya wakiwa na nia ya kujenga ushirikiano na wananchi haswa katika swala lizima la polisi jamii pamoja na ulinzi shirikishi .
Alisema kuwa kutakuwa na michezo mbalimbali ambayo itakuwa inashindaniwa ambapo alitaja kuwa ni mpira wa miguu ,mpira wa pete,riadha ,dhumna drafts(bao),kuvuta kamba pamoja na mpira wa mezani(pooltable).
Alisema kuwa kwakuwa wametambua kuwa uhalifu hauna mipaka na wala wahalifu hawana mipaka hivyo waliamua kuandaa mashindano haya wakiwa wanaamini kuwa yatasaidia kuvunja mipaka iliyopo kati ya vikundi mbalimbali vya ulinzi vilivyo katika mitaa na kata tofauti .
Andengenye aliongeza kuwa mashindano haya pia yataongeza mshikamano miongoni mwa vikundi kwa ujumla hivyo vitawanyima fursa wahalifu ya kupanga na kutekeleza vitendo vya uhalifu.
Alisema kuwa mbali na hilo michezo hii pia itasaidia kuwahamasisha wananchi hasa vikundi vya ulinzi shirikishi kujiunga katika miradi mbalimbali ikiwemo vikundi vya ujasiriamali kama vicoba pamoja na saccos.
Alimalizia kwa kutoa wito kwa wananchi kuunga mkono mashindano haya na kujitokeza kwa wingi katika mashindano haya ili yaweze kufana na pia alisema kuwa katika siku ya uzinduzi kutakuwa na vikundi mbalim
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia