MADARAKA BENDERA NA ALLY MOHAMMED WATEULIWA KUBEBA JAHAZI LA KUKINOA KIKOSI CHA MOUNT MERU WARRIORS

CHAMA cha soka mkoani Arusha(ARDF) kimewateua makocha wawili ,Madaraka Bendera na Ally Mohammed kubeba jahazi la kukinoa kikosi

Cha timu ya mkoa wa Arusha maarufu kama “Mt,Meru Warriors”katika michuano ya Kili Taifa Cup inayotaraji kuanz akutimua vumbi mnamo mwezi ujao.



Akihojiwa kuhusu maandalizi ya timu ya mkoa wa Arusha,katibu wa chama hicho,Adam Brown alisema kuwa chama hicho kimemteua aliyewahi kuwa mchezaji wa klabu ya Simba hapa nchini,Madaraka Bendera kuwa kocha mkuu akisaidiwa na Ally Mohammed ambaye ni kocha aliyeipandisha daraja katika ligi kuu klabu ya JKT Oljoro ya mkoani Arusha kutokana na vigezo mbalimbali walivyonavyo kikiwemo cha uzoefu.


“Chama cha soka mkoani Arusha kimewateua Madaraka Bendera kuwa kocha mkuu akisaidiwa na Ally Mohamed kukinoa kikosi cha Mt,Meru Warriors kutokana na vigezo mbalimbali ikiwemo experience(uzoefu) walionao”alisema Brown


Hatahivyo,Brown alisema kuwa tayari timu hiyo imesahaanza mazoezi yake ya kujiandaa na michuano hiyo ya Kili Taifa Cup katika viwanja vya shule ya sekondari ya Arusha Meru ulipo wilayani Arusha.


Aliwataka wakazi wa Arusha wakiwemo viongozi wa serikali mkoani hapa kujitokeza kwa wingi kuisapoti timu hiyo huku akisisitiza kwamba timu hyo siyo mali ya ARFA bali ni ya wakai wote wa mkoa wa Arusha.


“Wakazi wa Arusha watambue ya kuwa hii timu siyo mali ya ARFA bali ni mali yao,hivyo nawasihi wajitokeze kwa wingi kuisapoti timu yao”alisisitiza Brown

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia