Sunday, April 3, 2011
Posted by woinde on Sunday, April 03, 2011 in | Comments : 0
Mthamini wa mashindano ya Andengenye cup ambaye pia ni mkurugenzi wa RBP na pia ni balozi wa ulinzi shirikishi hapa nchi Rahma Alharooos akimkabithi kamanda wa polisi mkoani hapa Kombe ambalo mshindi wa mashindano hayo atapewa
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Thobias Andengenye akisoma risala mbele ya mthamini mkuu wa mashindano ya Andengenye cup
Balozi wa ulinzi shirikishi hapa nchini ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya RBP Rahma Alharoos jana wamekabidhi vifaa vya michezo pamoja na zawadi kwa kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha ambaye ameandaa mashindano yajulikanayo kama Andengenye Cup yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mapema April 9.
Akikabidhi vifaa hivyo balozi huyo alisema kuwa nia yao kama kampuni ya RBP ni kuthamini mashindano yate ambayo yameandaliwa na makamanda wa polisi wa mikoa mbalimbali hapa nchini.
Alisema kuwa hii ni mara ya pili kuthamini mashindano kama haya na mashindano ya kwanza waliyoanza kuthamini ni mashindano yajulikanayo kama Kova Cup ambayo yalifanyika jijini Dar es salaam.
Alisema kuwa wao kama RBP lengo lao kubwa la kuthamini mashindano haya ni kuwaweza wananchi haswa vijana kuweza kujiendeleza katika swala la ujasiriamali ,ulinzi na hata kuboresha miili yao kwa kucheza.
Alisema kauli mbiu yao ya mashindano haya ambao wameyathamini na wao ndio wanathamini wakuu inasema kuwa cheza Linda na ujasiriamali.
Alisema kuwa anapenda kuwasihi vijana wa mkoa wa Arusha kujitambua wao wenyewe na pamoja na kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi pasipo kuogopa kitu chochote.
Alisema kuwa japo kuwa vijana ndio damu inachemka na wanaweza kufanya kitu chochote wanatakiwa kujilinda kulinda amani iliyopo hapa nchini kwani iwapo wakiicheza ikitoweka kuirejesha itakuwa vigumu.
“kupitia michezo hii iliyoandaliwa na jeshi la polisi mkoani hapa basi vijana hawa wanaoshiriki watumie nafasi hii kushauriana na kukaa chini na kufikira jinsi ya kuendelea kuidumisha amani iliyopo kwani kutoweka kwa amani ni rahisi sana bali kuirejesha ni vigumu mno”alisema Rahma.
Alisema kuwa pia kampuni yao ya RBP inampango wa kuthamini mashindano haya yote yatakaofanyika katika mikoa yote hapa nchini ambapo alisema kuwa watagaramia zawadi zote ambazo na vifaa vyote vya michezo ambavyo vitatakiwa.
Balozi huyu wa ulinzi shirikishi walikabithi vifaa vya michezo vikiwemo jezi ,mipira pamoja na kombe la mshindi wa mashindano haya akisisitiza kuwa watakuwa bega kwa bega kushirikiana na kamanda wa polisi wa mkoani hapa adi mashindano hayo yatakapo malizika.
Rahma alisema kuwa pia kwakuwa yeye ni anapenda michezo na nimiliki wa timu ya African Lyion pia kupita mashindano haya atakuwa anachagua wachezaji wanaocheza vyema na kuwapeleka kucheza katika timu yake.
Alitoa wito kwa wakazi wa Arusha kujitokeza kwa wingi katika mashindano haya iliyaweze kufana kama walivyotaria akisitiza kuwa pia michezo ni burudani ivyo wakishiriki watakuwa ni njia moja wapo ya kujiburudisha.
Akipokea msaada huo kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Thobias Andengenye alisema kuwa anashukuru kwa msaada huo na kusema kuwa amefurahi kwa jinsi walivyowaunga mkoano na aliomba wananchi wajitokeze kwa wingi katika mashindano hayo ambayo alisema yatakuwa yanachezewa katika viwanja mbalimbali.
Mwisho.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia