BREAKING NEWS

Wednesday, April 27, 2011

MOSHI VETERANI WANYAKUWA KIKOMBE MOMBASA



Timu ya soka ya Moshi veterani katika picha ya pamoja mara baada ya
kufanikiwa kujinyakulia kikombe katika bonanza la Pasaka lililofanyika
mjini Mombasa hivi karibuni


TIMU ya soka ya Moshi veterani ya mkoani Kilimanjaro imefanikiwa
kujinyakulia kikombe na medali baada ya kuichapa timu ya soka ya
Nairobi water bao 1 kwa 0 katika mashindano ya bonanza la Pasaka
lililofanyika katika mji wa Mombasa nchini Kenya .

Katika Bonanza hilo linaloandaliwa na shirika la bandari la nchini
Kenya (KPA) kila mwaka,jumla ya timu sita zikiwa katika makundi
mawili, timu ya Moshi veterani ndio ilikuwa wawakilishi pekee kutoka
Tanzania .

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi zawadi kwa washindi
iliyofanyika katika uwanja wa mpira miguu wa KPA,Mwenyekiti wa timu ya
Moshi veterani Madesho Moye alipongeza waandaaji wa bonanza hilo kwa
zawadi zilizotolewa kwa washindi.

“Nitumie nafasi hii kupongeza uongozi wa bandari kwa zawadi,tumezoea
kuona zawadi kama hizi zikitolewa katika ligi kuu,na mashindano
makubwa huko ulaya,lakini ninyi mkaona japo tunacheza mpira umri ukiwa
umetupia tunastahili kupena vikombe na medali kwa hili niwapongeze
sana”alisema Moye.

“Kwetu sisi ni heshima kubwa sana mmetuonesha sina shaka hautuna budi
kuiga yote mazuri tuliyoyaona hapa KPA na kwa timu zilizoshiriki
pia”aliongeza Madesho.

Moye alisema timu ya soka ya Moshi veterani maarufu kama wazee wa
safari hawana budi kulingia zawadi ya kikombe na medali zilizopatikana
kutokana na kwamba ni timu chache Tanzania hususani za Veterani zilizo
pata mafaniko ukilinganisha na Moshi veterani.

Aidha Moye alisema lengo la kuanzishwa kwa timu ya Moshi veterani
linaelekea kutimia kutokana na mpango wake wa kutaka kusaidia
wachezaji wanaochipukia kupata nafasi ya kucheza soka nje ya nchi.

“Malengo yetu sisi kama Moshi veterani sasa yanaelekea kutimia kutoka
na urafiki tunaoendelea kujenga baina yetu na watu mbalimbali kupitia
michezo,tunao vijana ambao tunawalea wenyewe na ni wachezaji wazuri
tunahakika tutawaleta waje wasaidie timu ya Bandari inayoshiriki ligi
kuu ya Kenya.”alisema Madesho.

Katika bonanza hilo mchezaji Hassan Said wa Moshi veterani pia
alichaguliwa mchezaji bora ambapo alikabidhiwa zawadi ya kiatu cha
dhahabu huku timu ya Moshi veterani ikipata mualiko wa mashindano
mengine jijini Nairobi yatakayoandaliwa na Benki ya Bacrays.

Jumla ya timu sita zilishiriki katika bonanzo hilo ambazo ni
KPA,Manzili,West ham za mjini Mombasa ,Nairobi water na Bacrays za
Nairobi huku kutoka Tanzania ikiwakilishwa na timu ya Moshi veterani.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates