BREAKING NEWS

Wednesday, April 13, 2011

WASICHANA 216 WAKATISHWA MASOMO SABABU YA MIMBA

Wasichana 216 kutoka katika wilaya mbalimbali hapa za Mkoa wa Arusha wamelazimika kukatisha masomo yao mara baada ya kupata mimba wakiwa bado ni wanafunzi hali ambayo mpaka sasa inarudisha nyuma Maendeleo ya Elimu mkoani hapa hasa kwa mtoto wa kike

Hayo yalibainishwa na mkuu wa mkoa wa Arusha bw Isidore Leka Shirima wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na maendeleo ya mkoa wa Arusha.

Shirima alisema kuwa mimba hizo zilitokea kwa kipindi cha miaka mitano sasa ambapo watoto hao ambao walikatisha masomo hayo kutokana na ujauzito hali ambayo ililazimu mkoa kuchukua tahadhari mbalimbali

Aliongeza kuwa ndani ya kipinndi hicho wanafunzi hao walitokea katika maeneo mbalimbali ya mkoa ambapo ni pamoja na wilaya za Arusha vijijini, Arusha Mjini, Meru, Longido, Ngorongoro pamoja na wilayya ya Monduli

“sisi kama Mkoa tumechukuua hatua kali na za kisheria kwa wale ambao wamewapa ujauzito w atoto hawa wa kike ikiwa ni pamoja na kuwafikisha katika vyombo vya dola kama fundisho kwa wengine ambao wana tabia kama hii”alisema Bw Shirima

Akiongelea suala zima la maendeleo ya elimu mkoani hapa alisema bado mkoa unakabiliwa na changanoto mbalimbali za kielimu ambapo mpaka sasa kuna hatua mbalimbali ambazo zimeshatolewa na kuchukuliwa ili kuweza kukabiliana nazo

Shirima alisema kuwa moja ya changomoto hizo ni pamoja na uhaba wa Nyumba za walimu ambapo kwa sasa kuna uitaji wa nyumba za walimu 5446 sanjari na uhaba wa matundu ya vyoo ambapo kunaitajika matundu ya vyoo 6936 kwa mkoa wa Arusha .

Alisema kuwa changamoto nyingine ni pamoja na utoro wa wanafunzi hasa kwa jamii za wafugaji ambapo watoto wa jamii za kifugaji walio wengi bado mahudhurio yao ni hafifu sana .

Pia aliongeza kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi wa jamii za kifugaji wanakuwa watoro mashuleni kutokana na tatizo la wanafunzi hao kuishi mbali na makazi , pamoja na mwamko mdogo wa elimu ndani ya jamii zao jambo ambalo linasababisha elim u kuwa duni ndani ya jamii zao.

“jamii nyingi za wafugaji zimekabiliwa na changamoto mbalimbali hasa utoro lakini sasa sisi kama mkoa nalo tayari tumeshaanza kulifanyia kazi mojawapo ikiwa ni pamoja na kuanzisha vyakula mashuleni ili kuweza kupunguza tatizo la utoro mashuleni”alisema Bw Shirima

Aliwataka wazazi hasa wa jamii za kifugaji kuhakikisha kuwa wanatilia mkazo suala zima la elimu kwa kuwa kupitia kwao kunaweza kuongeza idadi ya wasomi ndani ya jamii zao.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates