BREAKING NEWS

Friday, April 15, 2011

KUMI WAFARIKI DUNIA AJALINI ARUSHA LEO

WATI 10 wamefariki dunia na wengine nane wamejeruliwa na wanne kati yao wanahali mbaya, baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongana na kupinduka katika eneo la Makumira wilaya ya Arumeru mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Arusha,Thobias Andengenye, alisema kuwa tukio hilo lilitokea leo majira ya saa 12:30 asubuhi katika eneo la Makumira nje kidogo ya mji wa Arusha.

Alisema kuwa ajali hiyo imehusisha gari aina ya Toyota hiece lenye namba za usajili T 773 BGT lililokuwa likiendeshwa na Selemani Juma (30)mkazi wa kijenge na Basi la Ngorika aina ya Scania lenye namba T 633 ANF lililokuwa likiendeshwa na Emanuel Mchoro(30) mkazi wa Mwanga kilimanjaro.

Kamanda Andengenye alisema kwamba chanzo cha ajali hilo kimetokana na gari aina ya haice kutaka kulipita gari lililokuwa mbale yake akiwemo mwendesha baiskeli ,hata hivyo kabla ya kufikia uamuzi huo aliona basi hilo la Ngorika likija kwa kasi na ndipo alipoamua kuingia porini ili kujinusuru asigongane uso kwa uso.

Hata vivyo kabla dereva huyo wa haice hajafika mbali ndipo gari hilo la ngorika lilimgonga ubavuni na kusababisha watu 9 waliokuwa ndani ya gari hiyo kufariki dunia papo hapo.

Andengenye aliwataja marehemu hao kuwa ni, Kizo Rafael Ndosi (35) mkazi wa Arumeru,Patriki Temba (28) mkazi wa Usariver,Samsoni Emanuel Minja (60),Hamisi Charles(30) mkazi usar river,John Kess(38) mkazi wa majichai,Huruma Safiel (28)mkazi wa usar river,Emanuel Mchoro (30) mkazi wa mwanga ambaye yeye ni dereva wa gari ya ngorika.

Mungine ni Fatuma Msuya (35)mkazi wa usar river ambaye yeye ndiye mwanamke pekee aliyekukfa katika ajali hiyo pamoja na dereva wa baiskeli aliyejulikana kwa jina moja la Elvisa.

Alisema mpaka sasa jeshi la polisi linamshikilia dereva wa gari ndogo (hiece)mpaka pale upelelezi utakapo kamilika.

Kwa upande wa Mganga mkuu wamkoa wa Arusha Salashi Toure alisema kuwa wamepokea majeruhi 16 ambapo kati ya hao mmoja amehamishiwa katika hospitali ya Seliani kutokana na mapafu yake kuonvujia damu nyingi.

"kwakweli mpaka sasa tumepokea majeruhi 16 ambapo kati ya hao mmoja tumempeleka katika hospitali ya seliani ili akapate matibabu huko"alisema Toure.






Watu waliojitokeza kushuhudia ajali hiyo


Baiskeli inayodaiwa kusababisha ajali




Mkuu wa mkoa Isdori shirima naye alifika katika eneo la tukio



wasamaria wema wakiwa wamebeba majeruhi




Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates