Thursday, April 7, 2011
BODI YA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO YATOA MSAADA WA NG'OMBE NA MBUZI
Posted by woinde on Thursday, April 07, 2011 in | Comments : 0
waandishi wa habari waandamizi kwa jina lingine wapiganaji maarufu wakiwa wa kushoto ni Jamila Omary na Kwame (marco Jaksoni) wakiwa wanarejea kwenye magari mara baada ya kushidwa kupita
ilifika mahali safari ikaishia hapo kwani tulikuta mto umefurika ikalazimika kurudi makwetu
kingine tulichokiona ni kwamba wakati wa asubui katika hifadhi ya ngorongoro kuna baadhi ya sehemu kunakuwa na ukungu mkubwa sana kiasi kwamba hatadereva haoni nainamlazimu kuwasha taa japo ni asubuhi
mwisho wa siku akabahatika kula
katika safari hii siku ya kwanza tulimkuta mzee wa pori Simba kapozi pembeni ya barabara tukamfatilia na haya ndio tuliyoyaona akiyafanya ndani ya hifadhi hii ya Ngorongoro
wakinamama pia walipatiwa misaada nao walijitokeza kusikiliza na kutoa malalamiko yao
mwenyekiti wa bodi akisikiliza risala ya wananchi
wananchi wawilaya ya ngorongoro wakiwa wanamsikiliza mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya ngorongoro Lukas Selelii wakati akiongea mara baada ya kukabidhi misaada ya ngombe na mbuzi
Jumla ya kaya 35 za wananchi jamii ya kimasai waishio katika wilaya ya Ngorongoro ambao ni maskini (Fukara) pamoja na wajane wamepatiwa msaada wa ng'ombe pamoja na mbuzi kwa ajili ya kujikwamua katika hali ya umaskini.
Akikabidhi msaada huo mwenyekiti wa kamati ya bodi ya hifadhi ya Ngorongoro Lukas Selelii alisema kuwa hifadhi ya Ngorongoro imeamua kutoa msaada wa ng'ombe wawili pamoja na mbuzi wa tano kwa kila kaya za wananchi wanaoishi katika mazingira magumu sana pamoja na wajane ili waweze kujikwamua katika hali ya umaskini pamoja na kujiendeleza kimaisha.
Alisema kuwa wao wameanzisha mkakati unaokusudia kubadilisha hali ya wamasai haswa katika kipindi hichi ambacho wamekataza kilimo katika eneo la hifadhi.
Alisema kuwa wameamua kuwapa ng'ombe hawa ili iwe ni njia moja wapo ya kilimo ambapo kufuatana na sheria inasema kuwa katika hifadhi hawaruhusiwi kulima bali kufuga ivyo ndio maana wameamua kuwapa ngombe hawa ili waweze kuwaendeleza na kuwakwamua katika hali duni.
Alibinisha kuwa wanampango wa kugawa mifugo hii katika wilaya yote ya ngorongoro haswa katika wale watu ambao wanaishi ndani ya hifadhi hii.
Alisema kwakipindi hichi walicho anza wanatarajia kutoa mifugo hii kwa jumla ya kaya 1000 ambapo hawataishia hapo kwani niya yao ni kutoa mifugo hii kwa wamasai wote ambao wanaishi katika hifadhi hii ya Ngorongoro.
Seleli alibainisha kuwa Mradi huu utasaidia pia kutoa elimu kwa wamasai kuweza kuwa na mifugo michache ambayo wataweza kuindeleza na kuifuga vizuri ambapo watatoa elimu ambayo itasaidia wafugaji hawa kufuga kwa kipindi kifupi zaidi.
''mradi huu utasaidia kuwapa elimu wafugaji kuweza pia kuacha kufuga mifugo mingi ambayo haina tija bali tutawaelimisha wafuge mifugo michache ambayo wataweza kutunza katika hali nzuri na itawasaidia kutunza kwa muda mfupi kama wa miaka miwili na kuwauza kwa bei ya juu"alisema selelii.
Alisema kuwa mradi huu unatarajia kutumia shilingili bilioni miatano za kitanzania ambapo katika hela hizo kutakuwa na fedha za kujenga kiwanda cha kusindika nyama za wafugaji hawa ambao watakuwa wameuza ngombe pamoja na kujengea kiwanda cha kusindika maziwa ambapo yatakuwa yamekusanywa kutokana na ngombe hawa ambapo hii itamsaidia mfugaji kupata soko kwa haraka.
"unajua nia yetu pia sio kuwapa tu hawa wafugaji ngombe bali kuwatafutia na sehemu ya kenda kuhuzia mifugo yao hivyo tukijengaa vitu hivi vitawasaidia mfugaji huyu kupata mahali pa kupeleka kwa haraka zaidi" alisema Selelii
Alisema kuwa mbali na hilo pia katika hela hiyo wanatarajia kujenga kujenga joshu la kunyweshea mifugo maji pamoja na kusafishia mifugo hiii katika kila kijiji.
Alitoa wito kwa wananchi hao ambao wanapatiwa mifugo hii kuweza kutoa ushirikiano zaidi ili waweze kufanikisha zoezi hili akiongeza kuwa mifugo hiyo waliyopewa waiendeleze na wajue kuwa hawajapewa bure bali wamepewa kutokana na fedha ambazo zinakusanywa katika hifadhi yao ya Ngorongoro.
Alitoa wito kwa viongozi ambao wanagawa mifugo hiyo kuhakikisha wanawapa walengwa bila ya kuwanyanya paa kwani wakiwanyanya paa watakuwa hawatendi haki kwa walengwa na sio kwao walengwa tu bali hadi kwa mungu.
"sisi tumetoa mifugo hii itolewe kwa wajane na wananchi ambao wanaishi katika mazingira magumu sana sasa nyie viongozi ambao tumewakabidhi naomba msiwachakachue bora mnichakachue mimi au meneja lakini sio hawa wajane kwani mtakuwa unatenda zambi hadi kwa mungu"alisema Selelii
Akipokea msaada huo mjane mmoja aliyejulikana kwa jina la Naishiye Elekuteka alisema kuwa wanaishukuru sana bodi hiyo na hifadhi kwa ujumla kwa kuwaona na kuwaletea msaada huo ambao alisema kuwa utamsaidia katika kujiendeleza katika maisha.
"msaada huu nitahakikisha nautumia vyema ili namimi niweze kujiendeleza mungu awabariki hawa wametuona hatuna uwezo wakatuletea nitauendeleza na nitaaakikisha natunza ngombe hawa hadi nije niuze milioni moja na nawahaidi kuendeleza huu mradi waliotupa jamani"alisema Elekuteka
Kamati hii ya bodi ya uhifadhi ambayo ilikuwa inaongozwa na mwenyekiti Juliasi selelii leo imetoa msaada wa ngombe na mbuzi katika kaya 35 ambazo zipo katika kijiji cha Oluptiro ambapo jumla ya vitongoji vitatu vimepatiwa misaada hiyo vitongoji hivyo ni Esere,Enduleti pamoja na Kakesio
na kila kaya wamepatiwa Ng'ombe wawili pamoja na Mbuzi watano .
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia