BREAKING NEWS

Wednesday, April 13, 2011

VIJANA 2000 WATIMUKA CCM ,KATIBU UVCCM ATHIBITISHA

Vijana zaidi ya 2000 wa chama cha mapinduzi ,kutoka katiika jimbo la Arumeru Mashariki wameamua kukihama chama hicho na kuhamia vyama vya upinzani kutokana na vijana hao kushindwa kutimiziwa maitaji yao muhimu ambayo waliahidiwa katika kipindi cha kampeni.



Hayo yamedhibitishwa leo na mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) , Christopher Palangyo wakati akiongea na viongozi wa kata 19 za jimbo la Arumeru mashariki wilayani humo



Christopher Alieleza kuwa hapo awali umoja huo ulikuwa na vijana wengi ambao walikuwa ni wanachama hai lakini kutokana na madhaifu mbalimbali yakiwemo ahadi hewa zilizokuwa kikitolewa , zimesababisha walio wengi kukihama chama hicho na kukimbilia vyama vya upinzani.



“Tunasikitika kusema kuwa tumepoteza vijana wengi sana kwa kuwa baadhi ya ahadi nyingi ambazo zilitolewa bado hazijatekelezeka na hivyo vijana wameona kuwa wanadanganywa hivyo wamekimbia chama hiki”alisema Christopher



Christopher aliendelea kwa kusema kuwa hali hiyo imekuwa ikiwasababishia adha kubwa sana ndani ya jamii ,ambapo wengi wa viongozi wa umoja huo wamekuwa wakizomewa pindi wapopita huku vijana hao wakidai ahadi walizoahidia kama vile kupewa mikopo .







“kwa sasa sisi hatuna imani kabisa kwa kuwa kila tunapopita tunaitwa matapeli wa ahadi na sisi tunapenda tu nafsi zetu na pia hii inazalilisha chama kwa kuwa orodha ya idadi ya vijana nayo inazidi kupungua siku hadi siku”alisema Bw Christopher



Pia alieleza kuwa baadhi ya viongozi walitoa ahadi mwaka 2007 ambapo ahadi hizo zilikuwa zikiwatia moyo vijana lakini hazikuweza kutekelezeka kwa wakati jambo ambalo mpaka sasa lin akimbiza vijana ndani ya kata hizo kwa kuamia na kurudisha kadi kasha kwenda upinzani.



Alieleza kuwa jambo hilo lina madhara makubwa sana ndani ya jamii ambapo kama uongozi wa chama hicho hautalichukulia maanani basi huenda wakakosa umoja huo w a vijana

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates