Sunday, April 3, 2011
MAJAMBAZI WATANO WAKAMATWA NA BASTOLA
Posted by woinde on Sunday, April 03, 2011 in | Comments : 0
Kamanda wa polisi mkoni hapa akionyesha bastola aina ya Bereta ambayo majambazo hao walikamatwa nayo
Jeshi la polisi mkoani hapa linawashikilia watu watano wanasadikiwa kuwa ni majambazi wakiwa wakiwa na silaha aina ya bastola.
Akiongea na waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoani hapa Thobias Andengenyeqa alisemqa kuwa watu hao watano walishikiliwa katika kijiji cha karanyi ambapo walikuwa wanataka kufanya uhalifu kwakutumia silaha.
Alisema kuwa watu hao wamekamatwa wakiwa na Bastola aina ya Bereta yenye namba H04757 ikiwa na risasi mbili ambapo alisema kuwa mmiliki rasmi wa silaha hiyo bado ajajulikana.
Alisema kuwa watu hao walikamatwa wakiwa wanataka kwenda kuvamia wanananchi wa kijiji cha kiranyi kilichopo wilayani Arumeru mkoani hapa.
Aliwataja majambazi hao kuwa ni Julius Laizer (22) mkazi wa Elkiurei ,Richard Martin (22) mkazi wa kiranyi Justin Likigerie (61)mkazi wa Kiranyi , Emanuel Zakaria (Manuu) mwenye umri wa miaka 23 mkazi wa kiranyi pamoja na Christopher Lovivi (25) mkazi wa kiranyi ambaye yeye ndiye aliyekutwa amebeba bastola hiyo.
Alisema kuwa uchunguzi wa awali ambao wameufanya jeshi la polisi pamoja na mahojiano ambao wamewahoji majambazi hao walibaini kuwa hili ni tukio la pili kwani majambazi hawa wanausishwa na tukio lingine lililotokea katika kijiji hicho hicho cha kiranyi mapema January 1 mwaka huu ambapo watuhumiwa hawa wanadaiwa kuvamia nyumba ya Jane Njau na kuiba vitu mbalimbali vikiwemo redio ,simu ,vidani vya golidi pamoja na fedha tasilimu.
Andengenye alisema kuwa bado watuhumiwa hawa wanashikili na upelelezi zaidi unaendelea na pindi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.
Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za watu wanaowashuku katika vituo vya polisi ili kuweza kuchukuliwa hatua mara moja kabla ya kufanya uhalifu au tukio lolote.
“habari hizi tumepata toka kwa wasamaria wema hivyo tunaomba wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi kutoa taarifa hizi ili mapema pindi tu wakiona watu hawaeleweki au wanawashuku kuwa ni waalifu”alisema Andenyenye.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia