Ticker

6/recent/ticker-posts

BAKWATWA WILAYA YATOA MSAADA KWENYE MASHINDANO YA ANDENGENYE CUP



picha katibu bakwata wilaya ya Arusha Abasi Mkindi (darueshi) akimkabidhi kamanda wa jeshi la polisi mkoni hapa Thobias Andengenye jezi pamoja na dawa za kutuliza maumivu


Baraza kuu la waislamu wa wilaya ya Arusha wametoa msaada wa jezi mbili pamoja na dawa kwa ajili ya maumivu kwa muuandaaji wa mashindano ya Andengenye Cup ambaye ni kamanda wa jeshi la polisi mkoni hapa.

Mashindano haya yaliyoanza Aprili tisa katika kiwanja cha kumbukumbu za sheikh wa Amri Abeid jijini hapa yanashirikisha timu zaidi ya 24 za mkoani hapa huku wadhamini wakuu wakiwa ni RBP .

Akikabidhi msaada huo kwa kamanda wa polisi mkoni hapa katibu mkuu wa bakwata wilaya mkoani hapa Abasi Mkindi Darueshi alisema kuwa wao kama bakwata wilaya wameona ni vyema wakiunga mkono mashindano haya kwa kutoa vifaa hivyo vichache .

Alisema kuwa wamefurahishwa sana kwa kitendo cha kamanda wa polisi kuandaa mashindano kama hayo kwani yatawasaida mambo mengi ikiwa ni pamoja na kuwaungani pamoja vijana wa mkoa wa Arusha pasipo kujali dini wala kabila.

"tumeona ni vyema tukawaunga mkono waandaaji wa mashindano haya kwani wameandaa mashindano mazuri sana ya kuwaeka pamoja vijana wetu bila kubagua dini kabila wala vyama vyao na kizuri zaidi wamewaweka pamoja ukiunganisha na hapo nyuma ambapo kuliuwa na vurugu na watu wakafikia kugombana lakini mashindano haya yamewaunganisha pamoja na wamepatana hivyo nawapongeza sana"alisema mkindi

Baraza hilo la bakwata wilaya ya Arusha wamekabidhi vifaa mbalimbali ikiwemo seti mbili za jezi pamoja na madawa ya kupunguza maumivu pindi mchezaji akiumia vyenye thamani ya zaidi ya shilingi laki tano.

Akipokea msaada huo kamanda wa polisi mkoni ha[a Thobiasi Andengenye alishukuru baraza hilo kwa kuona umuhimu wa kusaidia mashindano hayo ambapo msaada huo utaongeza hamasa kwa vijana.

Andengenye alisekuwa japo wamepewa msaada huu lakini bado mshindano haya yanakabiliwa na uhaba ukubwa wa vifaa vya michezo ikiwemo viatu,maji ,jezi ,mipira pamoja na Gloves na kuwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kuyasaidia mashindano haya ili yaweze kufana zaidi na zaidi.

Katika mashindano haya ambapo yanaendelea katika uwanja wa sheikh amri abeid jana timu ya kaloleni iliweza kuibuka kidedea mara baada ya kuwafunga timu ya polisi mkoa magoli 3-1 .

Post a Comment

0 Comments