WENYEVITI wa mitaa wametakiwa kujijengea utamaduni wa kuwa na kumbukumbu sahihi za wananchi wao ili kuwezesha shughuli mbalimbali za maendeleo kufanyika kwa uangalifu na umakini zaidi katika mitaa yao.
Mkuu wa wilaya ya Arusha, Raymond Mushi aliayasema hayo alipokuwa akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa anuani mpya na postikodi katika jiji la Arusha.
Mradi huo ambao umezinduliwa na Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) ulienda sambamba na utoaji wa semina kwa wadau mbalimbali wa mradi huo ambao ni madiwani, wenyeviti wa mitaa na wabunge kutoka manispaa ya Arusha.
Mushi alisema kuwa , kumekuwepo na changamoto kubwa sana ya wenyeviti wa mitaa kutokuwa na kumbukumbu sahihi za wananchi wao , hivyo kupelekea kutokuwa na ushirikiano wa kutosha pindi kunapohitajika namba sahihi za wananchi wake.
Aidha aliwataka madiwani kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuendeleza mradi huo ili wananchi wote waweze kunufaika ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuandaa bajeti katika vikao vya baraza ili kuwezesha mradi huo kufanikiwa kwa haraka zaidi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Haroun Lemanya alisema kuwa, wana mikakati madhubuti wa kuhakikisha kuwa wanafikisha mradi huo katika maeneo ya vijijini ili wananchi nao waweze kunufaika.
Alisema kuwa, mradi huo utamfikia kila mwananchi lengo kuu likiwa ni kila mwananchi kuhakikisha kuwa anakuwa na anuani mpya ya makazi ambayo itamwezesha kupata huduma za kiposta kwa urahisi zaidi .
Lemanya alisema kuwa, shirika la posta nchini lina jumla ya masanduku laki moja na sabini na tatu elfu ambayo bado hayajatosheleza kulingana na mahitaji ya wananchi kuwa ni kubwa sana hivyo kupitia mradi huo kila mwananchi ataweza kunufaika .
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia