wakwanza kushoto ni muaandaji wa bonanza la Afya kwanza akiwa na timu ya Triple a klabu Fc kabla ya mechi kuanza(habari picha na Woinde Shizza wa libeneke la kaskazini )
timu ya tigo Fc ikiwa pamoja na timu ya Triple A klabu FC
waimbaji wa bendi ya Ricker nest music band wakiwa katika picha ya pamoja na rais wa bendi hiyo alkievaa nyeupe
wachezaji wa timu ya Triple a wakiburudika mara baada ya mechi kuisha
waimbaji wa timu ya Ricker nest music band wakiwa na mmoja wa washabiki wao wa music wao wakifurahi pamoja
timu ya mringa ringa iikiendelea kufanya mazoezi kabla ya kuingia uwanjani
timu ya wavuta kamba ikiendelea kuvuta kamba
warembo wakifuatilia mpira kwa makini
timu ya Triple A wakiwa wanapeana mawazo katika kipindi cha mapunziko
wadau mbalimbali waliouthuria bonanza hilo wakiendelea kupata vinywaji
mmoja ya wachezaji wa timu ya Triple A klabu Fc akiwa anatolewa uwanjani na wauguzi mara baada yakuumia wakati akicheza
Timu ya Tigo Fc ikiwa katika picha ya pamoja kabla ya mechi baina yao na timu ya Triple A Klabu Fc kuanza
Na Woinde Shizza,Arusha
Timu ya Triple A klabu imelazimika kutoka sara ya bao moja
kwa moja na timu ya Tigo FC katika
bonanza la michezo lijulikanalo kwa jina la Afya Kwanza lililofanyika katika viwanja vya Gymkana
jijini hapa
Bonanza hilo ambalo
ni mara ya kwanza kufanyika limeandaliwa na
mkurugenzi wa Bendi ya Rickernest music band ,bendi ambayo makao makuu
yake ni jijini hapa na imeshirikisha michezo mbalimbali ikiwemo kuvuta
kamba pamoja na mpira wa miguu
Akiongelea bonaza hilo muandaaji wa mashindano hayo
Denis Mtedeki alisema
kuwa nia rasmi ya kuandaa bonanza hili ni kuwakutanisha watu mbalimbali na kufurahi pamoja pamoja na kushiriki michezo ,ikiwa kama ni sehemu ya kufanya mazoezi
Alisema kuwa bonanza
hili limeshirikisha jumla ya timu za mipira wa miguu mbili pamoja na timu
zingine mbili ambazo zilifanya kazi ya kuvuta kamba,alizitaja timu hizo kuwa ni
timu kutoka kampuni ya simu ya Tigo
(Tigo Fc), Olemringaringa FC, Red Apple,Mijada Fc pamoja na Triple a klabu FC.
Denis aliongeza kuwa
mbali na kushiriki bonanza hili pia wachezaji na washiriki waliouthuria
walipata fursa ya kupima magonjwa mbalimbali ikiwemo kupima presha na kisukari
bure.
Aidha aliongeza kuwa bonanza hili alitaishia hapa bali
litakuwa likifanyika kila mwisho wa mwezi lengo ikiwa ni kufanya mazoezi
,kuwakutanisha wadau mbambali mbali na kufurahi pamoja
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia