WATU 2 WAUWAWA NA MIILI YAO KUTUPWA KATIKA KATA YA KIKATITI
 

Watu 2 ambao bado majina yao hayajatambulika wenye umri wa miaka kati ya 40 na 50 wamekutwa wametupwa wakiwa wameuwawa katika kijiji cha Sakilakila kata ya kikatiti wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Taarifa mbalimbali za awali ziliwleza kuwa watu hao  walisombwa na mafuriko miili yao na kuburuzwa mtaroni jambo ambalo wakazi wa kijiji hicho wamesema eneo hilo halipitishi maji yenye uwezo wa kupoteza uhai wa mtu.

Lakini Kusaga News ilimtafuta mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Elifasi Marko Nko na kuthibitisha kukuta miili hiyo ya watu wawili waliouwawa na amesema kuwa watu hao hawakusombwa na maji bali wameuliwa wakaja kutupwa eneo hilo kulingana na muonekano wao kwa kuwa wote walikuwa wamerundikwa sehemu moja na hawakuwa wamechafuka kwa kuwa mtu akisombwa na mafuriko inajulikana na kuongeza kuwa siyo mara ya kwanza watu kutupwa eneo hilo wakiwa wameuwawa.

Mwenyekiti Nko amesema kuwa eneo hilo linafanywa kama jalala la kutuopa miili iliyokuwa ikishauwawa kutoka mbali na huku akieleza kuwa walipata taarifa za watu hao wawili waliokutwa wameuwawa baaada ya kuoneakana na mzee mmoja aliyekuwa anapita.

Naye Diwani wa Kata ya kikatiti bwana Elisa Stephano mungure amesema kuwa eneo hilo limekuwa walimkuta mwili mmojawapo kati ya hiyo miwili unatoa damu puani hivyo ikawapa wasiwasi na kukumbuka matukio ya nyuma ambayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara kwenye  kijiji hicho.

Juhudi za kumtafuta kamanda wa polisi zinaendelea

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.