MATUMIZI YA FEDHA ZA MFUKO WA MBUNGE ZAZUA SITAFAHAMU NDANI YA BARAZA LA MADIWANI

Madiwani wa halmashauri ya Meru wakiendelea Na kikao cha baraza kilichofanyika katika ilukumbi wa jengo la halmashauri hiyo


Diwani wa kata ya sambasha halmashauri ya wilaya ya Arusha  Mh Lengai  Olesabaya amehoji kuhusu fedha za mfuko wa mbunge jinsi zinavyotumika kwa wananchi wa jimbo.

Hayo yamejiri kwenye Mkutano wa baraza la madiwani kutajadili taarifa ya robo ya tatu ya mwaka wa fedha kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari - Machi, 2017 ambapo Diwani Lengai aliomba taarifa kuhusu mfuko wafedha zambunge zinavyotumika.

Akijibu hoja hiyo mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Arusha Noah Lembris amesema kuwa hoja hiyo haiwezi kujadiliwa kwenye baraza la adiwani kwasababu mbunge mwenyewe hakuwepo katika kikao hicho cha baraza hilo.

Kutokana na mvutano kati ya mwenyekiti wa halmashauri hiyo bwana Noah Lembris na Diwani  Lengai akalazimika kufunga mjadala huo kwa kuwa kwa mujibu wa kanuni amesema kuwa mbunge hawezi kujadiliwa kwasababu hakuwepo kwenye baraza hilo la Madiwani.

Hata Hivyo Diwani Olesabaya hakuridhika na majibu ya mwenyekiti wa halmashauri akamua kuomba tena muongozo wa kuomba majibu kuhusu mfuko wa mbunge na mwenyekiti akamjibu kuwa atapata majibu atakapo  kuwepo mwenyewe  mbunge

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.