Ticker

6/recent/ticker-posts

WAALIMU NA WANAFUNZI WILAYANI KONDOA WATAKIWA KUHAKIKISHA WANAFANYA VIZURI KWENYE MITIHANI YA TAIFA MWAKA HUU

Picha juu na chini Ni Mkuu wa wilaya ya Kondoa Bi Sezaria Makota akizungumza na wadau wa sekta ya elimu wilayani humo kwenye sherehe za Tathmini na motisha kwa waalimu wa shule za sekondari na msingi na wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya Taifa kwa mwaka jana Picha zote na mahmoud ahmad Kondoa


Pichani juu na chini kutoka kulia ni Afisa Elimu sekondari bi Hildacard Saganda,na Afisa Mipango Abuubakar kuuli na Mwisho ni mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Mwalimu Falessy Kibassa



Meza ya mbele ni waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Kondoa vijijini wakifuatilia kwa karibu Hotuba ya Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya hiyo Sezaria Makota

Mkuu wa wilaya Akitoa zawadi kwa mmoja ya waalimu walifanya vizuri katika kuhakikisha wanafunzi wanafaulu vizuri

Sehemu ya waalimu na wadau wa elimu wilayani humo wakifuatilia kwa ukaribu  matukio mbali mbali yalikuwa yakiendelea ukumbi wa Kondoa Irangi kwenye Maadhimishi ya shrehe za Tathmini ya kutoa zawadi kwa waalimu na wanafunzi waliofanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa mwaka jana

Juu na chini pichani  ni Mkuu wa wilaya akabidhi bendera nyekundu kwa waalimu shule za msingi na sekondari ambao shule zao zimefanya vibaya kwenye mitihani ya kitaifa na kutakiwa kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mitihani ya mwaka huu



Maafisa elimu Sekondari wakitoa zawadi za Vyeti kwa waliofanya vizuri 

Mmoja ya waratibu elimu kata Salumu Myeka wakifuatilia kwa makini wakiwa na wadau wenzake shughuli nzima ya utoaji wa zawadi


Mkuu wa wilaya ya Kondoa Sezaria Makota amewataka waalimu,watendaji na wadau  wa elimu wilayani humo kuhakikisha ufaulu wa wanafunzi unavuka lengo walilojiwekea sanjari na kuhakikisha maabara zinakamilika kwa wakati kwenye shule mbalimbali ili vifaa vya maabara walivyoahidiwa na wizara ya elimu wapewe kwa wakati.
Kauli hiyo ameitoa kwenye sherehe za tathmini ya sekta ya elimu wilayani humo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Kondoa Irangi wilayani humo.
Amesisitiza kuwa suala la kuwapati elimu watoto wilayani humo ni jukumu ambalo linahitaji ushirikiano wa wadau wote wa elimu wilayani humo na si suala la walimu pekee hivyo kwa umoja wao wanatakiwa kutoa ushirikiano ili kuweza kufanikiwa kufikia malengo katika sekta hiyo.
“Tumekuwa nyuma katika sekta ya elimu hivyo nawasihi wadau wote kuhakikisha wanafunzi wilayani hapa wanapata huduma muhimu ilikuweza kufikia malengo tarajiwa ya ufaulu wao na kuweza kuwa kwenye kumi bora za shule bora hapa nchini naahidi kulivalia njuga suala hilo ilikuweza kufikia malengo”alisisitiza Dc Makota.
Kwa Upande wake mkurugenzi wa wilaya Kondoa Vijijini Falessy Kibassa alisema kuwa atahakikisha kuwa suala hilo linafanikiwa lengo likiwa kuwawezesha waalimu na wadau kufikia malengo tarajiwa ya ufaulu na atalivalia njuga katika kuhakikisha masuala ya elimu wilayani humo yanakuwa ya mafanikio na mfano wa kuigwa mkoani hapa.
“Nasisitiza kutoa ushirikiano kwa wadau wa elimu na waalimu wilaya kwangu na milango ipo wazi kwa wadau kutoa maoni pale wanapoona kunalega katika sekta hii”alisisitiza Kibasa
Nae Afisa elimu msingi Alphonce Mwamwile alisema kuwa sekta ya elimu wilayani humo japokuwa inakabiliwa na changamoto kubwa za uhaba wa waalimu katika shule nyingi wilayani hapa pamoja na utoro,ukosefu wa chakula mashuleni wakati wa mchana watajitahidi kuhakikisha elimu inakuwa sanjari na ufaulu wa wanafunzi.
Afisa elimu Sekondari Hildacard  Saganda alisema kuwa kumekuwepo na changamoto kubwa ya umaliziaji wa maabara katika shule za sekondari hivyo kuwakosesha wanafunzi wanaojifunza masomo ya sayansi kukosa kujifunza kwa vitendo ila watahakikisha wanashirikiana na wadau wengine katika kutatua changamoto hiyo.

Kwa upande mwingine Mbunge wa Kondoa vijijini Ambaye pia ni naibu waziri wa Fedha na Mipango Ashatul Kijaji ameahidi kutoa Photocopy mashine kwa ajili ya mitihani ya kila mwezi kwa wanafunzi wa shule za wilaya hiyo



Post a Comment

0 Comments