WANANCHI WA WILAYA YA MERU WALALAMIKA KUKOSA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI


 


 Mahali pa Arumeru (kijani) katika mkoa wa Arusha
Wananchi wa wilaya ya Meru wamelalamikia ukosefu wa chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya wilaya hiyo jambo linalowalazimu kusafiri umbali mrefu mpaka hospitali ya Mkoa ya Mount Meru hivyo wameiomba serikali ijenge chumba hicho.
 
Wakizungumza  Wananchi hao wamesema kuwa wamekua wakipata usumbufu mkubwa hasa pale ndugu zao wanapofariki  na kukosa huduma hiyo ambayo iko mbali na maeneo hayo jambo ambalo linawagharimu hasa wananchi wengi wenye kipato cha chini.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Meru Ukio Kusirye amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo  ya ukosefu wa chumba cha kuhifadhia maiti licha ya idadi kubwa ya watu wanaohudumiwa
 
Kwa Upande wake Kaimu  Mkurugenzi wa Uendeshaji Mfuko  wa Hifadhi ya jamii ya NSSF  ,Bathow Mmuni amesema kuwa mfuko huo kwa kushirikiana na wadau wa sekta binafsi na serikali wataangalia namna ya kukabiliana na changamoto hiyo lakini kwa sasa wameamua kutoa mashuka 100 ili kupunguza adha ya upungufu wa vitanda ,magodoro na mashuka kwa kuwa mfuko huo umelenga kusaidia jamii

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF umekua ukujitoa katika kusaidia jamii hususan changamoto zilizoko katika sekta ya afya .

About Woinde Shizza

Mwandishi , Mjasiriamali na Mbunifu wa Mavazi. Email : woindeshizza@gmail.com , Instagram: woindeshizzablog.