Mwezi wa 9 katika kalenda ya kiislamu ni mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao ni maarufu zaidi kutokana na ibada ya Saumu.
Katika mwezi huu waislamu hutakiwa kufunga kutoka Machweo
mpaka Machwa (Mawio) katika kipindi ambacho hawatakiwa kula wala kunywa
chochote.
Mwezi wa Ramadhani ni muhimu kwa waumini was dini ya
kiislamu kwa kuwa ndio mwezi ulioteremshwa Kurani na pia hufahamika kama
mwezi wa Kurani.
Mbali na kujiepusha na kunywa na kula Muislamu hutakiwa
kujiepusha na maovu na matendo ya dhambi na kuongeza katika matendo ya
ibada kama Swala, Kusoma Kurani, kutoa sadaka na kadhalika.
Katika nchi nyingi duniani mwezi huu unaanza hivi leo tarehe 27 mwezi Mei mwaka wa 2017.