Na Leonce Zimbandu
MKURUGENZI
wa Manispaa ya Ilala, Msongela Palela ametoa cheti cha
shukurani kwa Mkazi wa Mtaa wa Kichangani kata ya Majohe, Gabriel
Macheho (pichani) baada ya kutambua mchango wake wakuhifadhi na kutunza rasilimali za umma.
Moja ya rasilimali hizo ni pamoja na kusimamia eneo
la umma lisichukuliwe na kumilikiwa na watubinafsi, likiwamo eneo
lamachimboyamchangalililokuwalikimilikiwanaMbezi Tile.
Afisa Uhusiano wa Manispaa hiyo,
Tabu Shaibu alimkabidhi Macheho cheti hivi karibuni kwa niaba ya Mkurugenzi ili kutoa motisha kwa wananchi wenye moyo wakutoa utetezi wa mali za umma.
Alisema Manispaa imeamua kutoa cheti hicho baada ya kutambua mchango aliotoa mkazi huyo kwa kufuatilia hadi kufanikiwa kupatikana kwa eneo hilo kwa ajili ya matumizi ya shughuli za kijamii,
ikiwamo ujenzi wa soko na shule.
“
Tunapaswa kuonesha uzalendo wakufuatilia mambo yenye manufaa kwa jamii ilikuishaidia jamii inayo kuzunguka,”
alisema.
Mkazi wa Majohe
Andrew Msuya alisema amefurahishwa na kitendo cha
Serikali kutambua mchango wa wananchiwachini, hiyo italeta chachu kwa watu wengine kuendeleza na kuhifadhi mazingira.
“
Naombaserikalikuendeleakuthaminimchangowawatuwachinikwakutoamotishailikukuzauhusianomzuri,”
alisema.
Gabriel
Macheho ameishukuru serikali kwa kutambua mchango wake
wa kutunza na kuhifadhi rasilimali za umma,
kwani wananchi wengi hawakujua kama huo ulikuwa ni wajibu wa msingi kutekeleza.
“Nitaendelea kutoa mchango wangu kwa serikali na jamii kwa ujumla ili kuhakikisha maeneo ya umma yanaendelea kulindwa na kuhifadhiwa,”
alisema.