Na Woinde Shizza, Kondoa
Wafanyakazi
wa Halmashauri ya wilaya ya Kondoa dc idara za Ulinzi,Madereva,watendaji Kata na
vibarua wanaolipwa kwa fedha za makusanyo ya mapato ya ndani wamemuomba waziri
wa Tamisemi George Simbachawene kunusuru kaya zao kwa kuingilia kati suala lao la malimbikizo ya
mishahara wanaoidai kwa miezi mitano
sasa ili kuwanusuru na hali ngumu ya kimaisha wanaokabiliana nao kwa sasa.
Wafanyakazi
hao waliongea na gazeti hili wilayani humo nakusema kuwa wanakumbana na hali
ngumu ya kimaisha inayosababishwa na wao kukosa fedha zao za mishahara kwa
miezi mitano sasa huku wimbo ukiwa ni suala lao lipo kwenye mchakato na miezi
inaenda.
Mmoja wa
wafanyakazi aliekataa kutaja jina kwa hofu ya kusimamishwa kazi kwenye idara ya
ulinzi alisema kuwa wamekuwa wakifuatilia fedha zao kwa kipindi kirefu huku
wakiambiwa mkurugenzi amekwisha saini dodoso la malipo yao lakini wao mpaka leo
hawajalipwa chochote hiyo imekuwa ikiwawiya vigumu katika hali za kimaisha
mjini.
Amesema kuwa
mjini unakuwa umepanga nyumba una watoto unasomesha wanahitaji chakula na
mahitaji mengine sasa unafikiria utaishi vipi kwa hali tunamuomba waziri Tamisemi
kuingilia kati kuweza kulipwa fedha zetu kwani mamlaka zote ngazi ya wilaya
wanalijua suala letu bila majibu wala kupata stahiki zetu tena ambazo
tunazivujia jasho usiku na mchana.
Kwa upande
wake mmoja wa vibarua amesema kuwa fedha zao wanazodai katika halmashauri hiyo
imekuwa ni usumbufu na kila wanapokwenda kwa Mhazini wa halmashauri madai yake
fedha hakuna fedha hivyo wao kuendelea kuishi katika hali ngumu ya kimaisha na
huku familia zikiwategemea.
“Sisi
tunamuomba sasa waziri simbachawene kulifuatilia suala letu kwani tunaimani na
serikali ya awamu ya tano katika kuwajali wanyonge na watu wa kipato cha chini
hivyo tunaamini atalishughulikia”aliongeza mfanyakazi huyo