Mkuu wa mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera akifatilia jambo wakati alipokuwa anazindua rasmi maonyesho ya sita ya vito na madini yanayofanyika katika hotel ya Mounti Meru ilipo jijini Arusha(habari picha na Woinde Shizza,Arusha)
Meya wa jiji la Arusha naye aliuzuria katika uzinduzi wa maonyesho haya ya vito na madini
Na Woinde shizza,Arusha
Wananchi wengi wanaoishi karibu na migodi
mbalimbali inayochimba madini ya aina
mbalimbali wamekuwa hawanufaiki kupitia madini hayo kutokana na viongozi wao wa
maeneo husika kutokuwa na usiano mzuri
na wamiliki wa migodi hiyo.
Hayo yamebainishwa na mbunge wa jimbo la Simanjiro Jemsi ole
milya wakati akiongea katika uzinduzi wa maonyesho vito na madini yaliofunguliwa leo jijini hapa
Alisema kuwa japo kuwa madini mengi yenye dhamani yanachibwa
hapa nchini lakini ukifuatilia maisha ya wananchi wa maeneo ambayo madini hayo yanatoka hayafanani
kabisa nao kwani asilimia kubwa ya wananchi hao ni maskini sana na wengine awajiwezi
“asilimia kubwa ya
wananchi ambao madini hayo yanachibwa ukifatilia maisha yao hayafai kwani ni
duni hawana maendeleo yoyote ,kwa ufupi awanufaiki na madini ambayo
yanatoka katika maeneo yao hivyo ni wajibu waserikali kuangalia upya swala hili
na kuanza kufatilia kwani ni kitu cha kusikitisha unakuta mwananchi mfano wa Mererani madini yanachibwa kwao lakini ukiangalia maisha anaoyoishi uwezi sema
anakaa sehemu Tanzanite inatokea kwa jinsi anashida”alisema Milya
Naye kaimu naibu
katibu mkuu wa wizara ya Nishati na madini Jemsi Mdoe alisema kuwa sera ipo na sheria ipo ya
kuakikisha wananchi ambaowanazunguka maeneo ya migodi wanasaidiwa na migodi hiyo lakini ukifuatilia kwa kiasi
kikubwa wale wananchi ambao hawanufaiki ni wale ambao unakuta viongozi wao wa
mtaa au kijiji awanaushirikiano mzuri na viongozi au wawekezaji waliowekeza
katika maeneo yao ,hivyo ni wajibu wawanchi pamoja na viongozi kushirikiana kwa
pamoja na kuungana ili kuweza kusaidia
Akizungumzia maonyesho haya ya madini ya vito (Arusha Gem Fair )alisema kuwa haya ni
maonyesho ya sita kufanyika na yanafanyika kwa muda wa siku tatu lengo ikiwa
kutimiza dira iliopo katika sera
ya madini ya mwaka 2009 inayosisitiza
kuwa Tanzania iwe kitovu cha madini .
Alisema kuwa sekta ndogo ya vito inachangia katika uchumi wa
maendeleo ya jamii hivyo maonyesho
haya ni fursa kwa wachimbaji na wafanyabiashara wa hapa nchini kuweza
kupata fursa ya kujitangaza zaidi
“unajua wageni wengi
kutoka nchi mbalimbali wanauthuria katika maonyesho haya wengine wanakuja
kununua madini wengine wameleta madini yao ili yauzwe kwaiyo hii ni fursa ya
pekee ya wachimbaji wetu wa ndani kujitangaza na kupanua soko la zaidi kikubwa
zaidi waangalie ni namna gani
watayafanya madini yao yawe na dhamani zaidi”alisema Jemsi
baadhi ya madini yaliyoletwa katika maonyesho
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia