Mwanamziki Kamanda Ras Makunja na mzimu wake Ngoma Africa Band
Mziki wa dansi Kutoka Uswahili hadi kimataifa Ujerumani na ulaya,
Tunapozungumzia
muziki dansi wa Tanzania "Bongo Dansi" kuvushwa na kufikishwa katika
majukwaa ya kimataifa jina la mwanamuziki mtanzania Kamanda Ras Makunja
na bendi yake The Ngoma Africa Band hatuwezi kulikwepa.
Mwanamuziki
wa kitanzania kamanda Ras Makunja mtunzi,mwimbaji,kiongozi na
mwanzilishi wa bendi maarufu Ngoma Africa band aka FFU au viumbe wa
ajabu "Anunnaki Aliens" yenye makao yake nchini ujerumani,bendi
inayodumu
kwa takribani miaka 29 tangu aianzishe mwaka 1993
kwa madhumuni ya kuitangaza nchi Tanzania kimataifa kwa kupitia njia ya
muziki wa dansi na kujizolea washabiki na tuzo za kimataifa,ikiwepo tuzo
ya bendi bora ya kigeni iliyodumu kwa muda mrefu barani ulaya "Best Diaspora Band Award" sio
jambo rahisi kwa bendi ya kigeni tena ya kiafrika kuweza kuimili na
kudumu kwa zaidi miongo miwili barani ulaya na bendi nyingi za kigeni
zimeshindwa kutimiza hata mwaka moja lakini mtanzania mwamba huyu Ras
Makunja ameweza kuongoza mzimu wake Ngoma Africa Band na kufanikiwa
kuwanasa malfu ya washabiki na kuitangaza Tanzania.
Mwanamuziki huyu Kamanda Ras Makunja ni nani haswa ?
mwanamuziki mwamba huyu nguli jina lake haswa alilopewa na wazazi wake ni
Ebrahim Jumanne Salehe Makunja alizaliwa Dar es salaam ni mtoto wa mwanzo wa Bw.Jumanne Salehe Makunja na Bi.Mozah Hassan Mpili.
inasemekana wazazi wake walimpeleka kupata elimu akiwa na umri mdogo
katika shule ya kinondoni,osterbay na elimu ya kati Kibasila na kupata
mafunzo ya masoko na biashara katika tahasisi ya Impex iliyopo
Birmingham uingereza na baadaye North-West Europe business Zentrum kule
Heldesheim ,Ujermani,anaongea lugha nne za kimataifa
Kijerumani,Kingeleza,Patois na kiswahili kutokana na vipawa hivi wenzetu
wa jerumani walimgundua kuwa huyu ni madini wakampa ugali wa kuwa
mtaalam anayeshughulikia
Conseling kwa watoto na vijana katika kituo cha
JugendKultur Zentrum katika mji wa Oldenburg kituoa ambacho kinatoa
ushauli kwa watoto na vijana katika shughuli za sanaa,elimu na
muziki,ambapo alifanikiwa kuifanya kazi ya kuokoa vijana zaidi ya elfu
sita walikuwa wanasumbua mitaani baada ya shule katika mji wa
Oldenburg,kazi ambayo polisi wa jiji walishindwa kuifanya kwa ajili ya
kutumia nguvu lakini Kamanda Ras Makunja aliifanya kwa kutumia mbinu
ambazo wajerumani waliziita (Psychologist) na kumtaja mwamba huyu kuwa
ni kiumbe wa ajabu the Alien mwenye mvuto wenye ushawishi mkubwa.
Ras
Makunja ni mume na baba familia yake ni kitanzania,Ras Makunja bado
raia wa Tanzania pamoja na kuwa mara nyingi ameombwa kuwa raia wa
ujerumani lakini amekataa anaishi ujerumani kwa muda wa miaka 28 sasa na
kupata hati ya mkazi wa kudumu.
Safari yake ya maisha ya muziki ilianzia mapema sana akiwa na umri mdogo
akiwa
katika vikundi vya kwaya ya shule na kufanikiwa katika umri mdogo akiwa
shuleni kinondoni kujiunga na kwaya maarufu wakati huo ya Umoja wa
Vijana wa chama cha TANU (TYL) Tanu Youth League iliyokuwa inaongozwa na
mzee Makongoro,kwaya hiyo ilikuwa na utaratibu wa kuchukua watoto wenye
vipaji kutoka mashuleni na kuimba nao,lakini wazazi wa
Makunja walikuwa
makini na wakali sana katika kuhakikisha mtoto wao anapata elimu ya
kutosha kuliko kutekwa na sanaa ya muziki na walifanikiwa katika
hilo,pamoja na hayo mtoto wao yaani kamanda Ras Makunja naye alifanikiwa
ndoto yake ya muziki mwaka 1978 alijiunga kwa muda mfupi na Butiama
Jazz iliyokuwa inamilikiwa na marehemu Mustafa Mkwega baadaye alitoka
kutokana na alipata ajira iliyokuwa
ngumu kugawa muda wa
muziki na kazi,ajila hiyo ilikuwa kati ya Mazimbu Morogoro na Dar Es
Salaam kuudumia wapigania uhuru wa kusini mwa afrika.
Baadaye
alijiunga na kundi la Roots and Culture liliongozwa na marehemu Jah
Kimbute Mleteni bendi ambayo nayo ilitumika sana katika harakati za
kupigania uhuru wa kusini mwa afrika,bendi hiyo ndiyo iliyokuwa
inazungua katika nchi sita zilizo mstali wa mbele (Frontline States)
bendi hiyo nayo iliweza kutembea katika kila nchi na kuwafikiwa
wapigania uhuru na kuwatia hamasa.
Ras Makunja kuanzia 1990 alipaata
fursa ya kuanza kusoma kijerumani Goithe Institut Dar na kupata fursa ya
kuchaguliwa katika timu watafiti iliyoundwa na wajerumani na
watanzania kuhusu utamaduni na utalii (Tourist Impact of
Tanzania).
baadaye akaondoka katika kundi la muziki la Roots and Culture
na kuhamia nchini Ujerumani kujiendeleza kielimu na akafanikiwa
kuanzisha bendi yake Ngoma Africa Band mwaka 1993 ikapata udhamini wa
project ya "We are One" wazunguka kupiga muziki Ujermani yote kwa
kupinga ubaaguzi wa rangi ambao miaka ya 1990s ulikuwa umeshika
kasi.makunja na bendi yake walifanikiwa kubadilisha fikira za vijana wa
kijerumani wengi kwa kupitia silaha ya muziki wa dansi ambao hapa
Tanzania hauna thamani.
Mwaka 2000 aliingoza bendi yake katika maonyesho ya World Expo 2000 Hannover,
tarehe 8.08.2000 katika malumbano ya jukwaani mwamba Kamanda Ras
Makunja na bendi yake aliipaisha Tanzania kimataifa na kuchaguliwa kuwa
The Best Worldmusic band of Expo 2000 Hannover.mwaka 2001 Makunja
aliongoza bendi yake at "Pacific World Music Festival Honolulu,Hawai.
Mwaka
2007 Fiesta Latina ,Caracas Venezuela.Mwaka 2010 Ras Makunja na mzimu
wake ndani ya Finland, mwaka 2011 Ras Makunja na bendi yake akaingia
Serbia,Bosnia ambako si nchi rahisi kutokana kuwa nchi hizo zilikuwa
zimetoka kwenye vita,mwaka huo huo 2011 Kamanda Ras Makunja na bendi
yake walipata mwaliko wa kwenda Libya lakini serikali ya Ujerumani
ilizuia bendi hiyo kwani hali ya Libya haikuwa shwali.Mtanzania huyu Ras
Makunja mwaka 2014 na bendi yake walialikwa kwenda kutumbuiza katika
sherehe za miaka 60 ya taifa la Israeli wakafanikiwa kutingisha katika
uwanja wa Isaack Rabin Square mjini Tel-Aviv.
Kamanda Ras Makunja mkuu wa kikosi maalumu The Ngoma Africa Band au the FFU-Ughaibuni almaarufu pia kama viumbe wa ajabu "Anunnaki Aliens" akipanda
jukwaani ni kazi moja tu kuwadatisha maelfu ya washabiki katika
maajukwaa ya kimataifa na kuipeperusha tanzania.Ras Makunja
mwimbaji,mtunzi pia social commentator mwenye kutunga nyimbo za kuelimisha na kugusa jamii zikiwe CDs kama "Rushwa Ni adui wa Haki"
CD:Mama Kimwaga ,CD: Apache wacha Pombe, CD;Miaka 50 ya Uhuru
na nyingi nyinginezo.Kamanda Ras Makunja mtoto wa Tanzania aliyejitoa muanga kuipeperusha bendera ya Tanzania kimataifa.
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia