Ticker

6/recent/ticker-posts

TEMDO YABUNI MTAMBO MDOGO WA KUTENGENEZA SUKARI UTAKAO WEZA KUAJIRI VIJANA ZAIDI YA 100



Meneja huduma za kihandisi viwandani  Mhandisi Jackson Massaka  akiwa ameshikilia zawadi ya kikombe cha mshindi wa pili katika nafasi ya ubunifu wa mashine na zana za kilimo waliopewa katika maonyesho ya 28 ya wakulima na wafugaji yaliyofanyika katika viwanja vya themi njiro ndani ya halmashauri ya jiji la Arusha 

 Taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo nchini (TEMDO)imebuni mtambo mdogo wa kutengeneza sukari utakao weza kupunguza tatizo la ajira kwa vijana na kuweza kujiajiri wenyewe.


Akiongea mara baada ya kupokea zawadi ya kikombe cha mshindi wa pili katika nafasi ya ubunifu wa mashine na zana za kilimo Meneja huduma za kihandisi viwandani Mhandisi Jackson Massaka alisema kuwa Temdo wapo potepote kwenye kutoa huduma mbalimbali za sekta ya Kilimo pamoja na sekta ya afya Kwa upande wa Vifaa tiba 




Alisema kuwa mtambo huu mdogo unauwezo wa kutoa ajira zaidi ya 150 za moja Kwa moja na kutoa ajira 1800 zisizo kuwa za moja kwa moja Kwa ajili ya vijana wa kitanzania.



Alisema kuwa wameona ni vyema kubuni mtambo huu ilikuweza kusaidia kuongeza ajira kwa vijana ambayo imekuwa ni changamoto kubwa linalowakabili vijana ,ambapo alifafanua kuwa mashine hii itawasaidia kuweza kujiajiri na hata kuwaajiri wengine.


"Sisi kama temdo tumejikita kutengeneza mashine hizo Kwa ajili ya mkulima Ili kuhakikisha mkulima anapolima anaongeza tija katika mazao yake pia anazalisha vizuri na kwafaida huku akilima kilimo biashara "alisisitiza 



Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko katika taasisi hiyo,dkt Sigisbert Mmasi alisema katika maonyesho haya ya nane nane wameweza kuleta mashine mbalimbali Kwa ajili ya kusaidia wakulima pia wameweza kuwaeleza faida za kutumia mitambo hiyo.


"Tumeweza kupata kikombe hiki sio tu kwa vile sisi ni taasisi ya serikali hapana bali ni kwa vile tunajitahidi kutoa huduma bora na hatutaishia hapa tutaendelea kusanifu mitambo kwa ajili ya kusaidia wakulima ,na tutaendelea kutengeneza vifaa tiba Kwa ajili ya hospital zetu na kwa ajili ya kupunguza gharama kubwa za uagizaji nje vifaa hivyo nje ya nchi"alisema Mmasi



Alisema kuwa mtambo una uwezo wa kuchakata miwa ya sukari tani 200 na kutoa sukari tani 20 Kwa siku.


Alisema kuwa, mbali na mashine hii pia wameweza kubuni machine ya kuchakata zao la zabibu ambapo alisema kuwa wakulima wamekuwa wakipeleka zabibu zao Moja Kwa moja kwenye viwanda vya mvinjo(wine) na wanapopeleka wamekuwa wakipewa fedha kidogo ,lakini mkulima anapokuwa na mashine hii ataweza kuongeza dhamani zao lake na litampelekea kupata fedha nyingi.


Alisema mashine hiyo ina uwezo wa kutoa lita 700 hadi 800 kwa saa ya mchuzi wa zabibu .



Baadhi Wafanyakazi wa Taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo nchini (TEMDO) wakiwa katika picha ya pamoja wakishereke ushindi mara baada ya taasisi yao kushika nafasi ya pili wa wabunifu bora wa mashine na zana za kilimo katika maonyesho ya 28 ya sikukuu za wakulima na wafugaji zilizofanyika katika viwanja vya Themi Njiro mkoani Arusha jana(

Post a Comment

0 Comments