BREAKING NEWS

Tuesday, August 9, 2022

RAIS SAMIA MGENI RASMI KATIKA MKUTANO WA 44 WA SHIRIKISHO LA SOKA AFRIKA

 



 

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa  wa 44 wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) utakaofanyika kesho agost 10 katika ukumbi wa mikutano wa AICC Jijini Arusha.

 

Akizungumza na waandishi wa habari, Rais wa Shirikisho la soka Tanzania Walence Karia amesema mkutano huo utajumuisha jumla ya wageni 400 wakiwemo wajumbe halali 156 kutoka nchi 52 wanachama wa CAF.

 

kutoka kushoto Rais wa shirikisho la soka Tanzania Wallace Karia akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu mkutano wa CAF, anaefuata ni mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela na mkurugenzi wa michezo nchini Yusuph Siungo

“Nchi wananchama 54 lakini Kenya na Zimbabwe wameondolewa kwenye mkutano kutokana na serikali ya nchi hizo kuingilia shughuli za michezo”

 


Rais Karia alisema katika mkutano huo mbali na wajumbe watakuwepo wageni wengine watakaokuwepo ni pamoja na Rais wa shirikisho la mpira duniani ‘FIFA’ Gianni Infantino ambae nae amemualika Rais wa shirikisho la soka Qatar kuwakilisha bara la Esia pia rais wa Shirikisho la soka barani Afrika (Caf) Patrice Motsepe atakuwepo na wachezaji wa zamani maarufu”

 

Alisema kuwa ajenda kuu ya mkutano huo ni kupokea taarifa za maendeleo ya mpira wa miguu, taarifa za fedha sambamba na kujadili uanzishwaji wa mashindano ya ‘Afrika Super cup’

 

‘Tukifanikiwa kukubaliana na kupitisha kwa pamoja mashindano haya yaanze tunatarajia Yatatuzinduliwa rasmi hapa Arusha”


Alisema kuwa pia watajadili  mashindano mbali mbali ikiwemo klabu bingwa Afrika ‘Afrika championship’ na mashindano ya shirikisho lengo ikiwa ni kupata fedha za kusaidia kuendesha mashirikisho ya mpira.

 

Kwa upande wake mkurugenzi wa michezo nchini, Yusuph Singo alisema kuwa maandalizi yote kuelekea mkutano huo yamekamilika na wageni wameshaanza kuingia ambapo Rais wa FIFA anatarajiwa kupokelewa jioni katika uwanja wa kimataifa Kilimanjaro KIA.

 

“Mkutano huu umekuja kutokana na mahusiano na mashirikiano mazuri tuliyonayo na shirikisho letu, hivyo serikali itaendelea kutoa sapoti kubwa ili michezo nchini iendelee kukua ikiwemo kuboresha viwanja viwe na hadhi ya kimatafa ili tuweze kupata mashindano makubwa”

 

Nae mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela aliwahakikishia wageni wote ulinzi wa kutosha kwa siku zote watakazoishi mkoani Arusha na mashirikiano huku akiwataka wakazi wa Arusha kuwa wakarimu kuwasaidia wageni watakapohitaji msaada.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates