Ticker

6/recent/ticker-posts

WANANCHI WA JIMBO LA SAME MASHARIKI WAONDOKANA NA HADHA YA KUSAFIRI MDA MREFU KUFUATA HUDUMA YA MOCHWARI

 

WANANCHI wa jimbo la Same Mashariki wilayani Same mkoani Kilimanjaro wataondokana na hadha ya kusafiri umbali wa kilomita 75 kufuata huduma ya uhifadhi wa miili ya marehemu wao (mochwari) katika hospitali ya wilaya baada ya Serikali kuweka jokofu ya kuhifadhia miili hiyo kituo cha Afya Ndungu.



Hatua ya kufungwa kwa jokofu hilo lenyeuwezo wa kuchukua miili sita limefikia baada ya Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kasimu Majaliwa kufanya ziara katika jimbo hilo Septemba 24 mwaka jana na kupokea changamoto hiyo na kuahid Serikali ingetatua.





Mbunge wa Jimbo hilo, Anne Kilango Malecela alisema kuwa, wananchi hao wamekuwa wakitumia gharama kubwa kuhifadhi ndugu zao ambao wametangulia mbele za haki huku wale ambao wamekuwa wakishindwa  kumudu  gharama hulazimika kutumia njia za jadi kuhifadhi ambazo sio salama.




"Katika jimbo langu lote hakukuwa na huduma ya kuhifadhi miili za marehemu ambapo wananchi wangu walikuwa wanalazimika kwenda Korogwe mkoani Tanga kilomita 70 au kwenda hospitali ya wilaya ya same kilomita 75 kupata huduma ya kuhifadhi marehemu " alisema Anne Kilango. 





Alisema kuwa, kupatikana kwa huduma hiyo ya mochwari katika kituo cha Afya Ndungu kutawapunguzia kero kubwa kwani wamekuwa wakitumia gharama kubwa.




Aidha Mbunge huyo alitumia nafasi hiyo kumshukuru Waziri Mkuu Majaliwa na Serikali ya CCM kuona kero hiyo kubwa ambayo ilikuwa ni takwa la wananchi wa jimbo la Same Mashariki. 




Kwa upande wake, Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Ndungu, Dkt . Tatizo Mwakatuya alisema kuwa, awali walikuwa na jengo la mochwari katika kituo hicho lakini hawakuwa na jokofu la kuhifadhia miili na kwa sasa wamepokea  jokofu lenye uwezo wa kuhifadhi miili sita lenye gharama ya milioni 17 na limeshaanza kufanya kazi.



Dkt. Mwakatuya alisema kuwa, kituo hicho cha Afya kinahudumia Kata tano ambazo ni Bendera, Kihurio, Kalemawe, Gonja na Miamba hivyo kupatikana kwa mochwari ni mkombozi  mkubwa.





Alisema kuwa, kwa sasa kituo hicho kinakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa gari la kubebea  wagonjwa ambapo Mbunge ameahidi kulifwatilia liweze kutatuliwa na Serikali. 



Post a Comment

0 Comments