BREAKING NEWS

Tuesday, August 2, 2022

WAZIRI AWESO ASHUSHA BEI YA MAJI KARATU,ASEMA SERIKALI YATOA BILIONI ZAIDI YA NNE KUMALIZA KABISA KABISA TATIZO LA MAJI KATIKA MJI HUO

waziri wa maji Jumaa Aweso akiongea katika kikao kazi cha kusikiliza maoni ya wananchi na wadau mbalimbali wa maji wakiwemo madiwani na wabunge wilayani humo  


Mkuu wa wilaya ya Karatu Dadi Kolimba akiongea katika kikao hicho


diwani kata ya Qurus Danstan Panga  akitoa maoni katika kikao kazi  hicho 


Na Woinde Shizza , ARUSHA

Rais wa jamuhuri wa Tanzania amekubali kutoa kiasi cha shilingi bilioni 4.5 kwa ajili kujenga mradi mkubwa wa maji utakao weza kutatua tatizo kubwa la maji ndani ya wilaya ya Karatu mkoani Arusha.

Hayo yameelezwa na waziri wa maji Jumaa Aweso wakati alipofanya kikao kazi cha kusikiliza maoni ya wananchi na wadau mbalimbali wa maji wakiwemo madiwani na wabunge wilayani humo

Aidha pia waziri katika kikao hicho aliweza kumaliza mgogoro wa bei za kuuza maji uliodumu kwa muda mrefu wilayani Karatu baada ya kutoa maagizo ya kuwepo kwa chombo kimoja kitakachosimamia utoaji wa huduma ya maji katika mji huo huku akiagiza bei ya maji inayostahili kutozwa kwa sasa ni sh1,300 kwa uniti1 badala ya sh2,000 hadi sh 3,000 kwa unit moja.

Alisema kuwa Rais aliameona tatizo la upatikanaji wa maji katika mji huo ndio maana akaweza kurithia kutoa kiasi hicho cha pesa kwa ajili ya kumaliza tatizo hilo,ambapo pia alitumia muda huo kutoa maagizo kwa mamlaka husika kuanzia kutangaza zabuni ya mkandarasi atakae tekeleza mradi huo wa kusambaza maji haraka

"Huu mgawanyiki wa maslahi kaviwasu na kaviwasa unatakiwa uhishe ili wananchi waweze kupata huduma bora za maji mnavyouza maji bei hizo mnawaumiza wananchi mfano kaviwasa kutoza shilingi 2000 hadi efu 3000 kwa unit moja ambayo ,nisawa na ndoo 50 za Lita 20 haikubaliki serikali aitakubali kuona mwananchi wake anaumia hivyo naagiza kwamba kuanzia Sasa unit 1 iuzwe Bei sawa na halmashauri ya jiji la Arusha ya shilingi 1300 katika kipindi hicho ambacho Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji( Ewura) inapoendelea kuchakata bei halisi itakayotozwa kwa wananchi juu ya ulipaji wa ankara za maji"alisema Uweso

Kutokana na mkanganyiko huo wa kuingiliana kwa vyombo viwili vinavyotoa huduma ya maji katika mji wa karatu waziri huyo alivitaka vyombo hivyo ambavyo ni Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Karatu (KARUWASA) na Mamlaka ya Utoaji wa Huduma ya Maji Vijijini (KAVIWASU) kuungana na kutengeneza chombo kimoja ambacho kitatoa huduma bora kwa wananchi .

Aliwataka kuweka utaratibu wa kumtangaza mkandarasi Ili aanze kazi ya kusambaza miundombinu ya maji na huku wao wenyewe wakianza kuunda bodi itakayopanga mipango yake kwani maji si biashara bali ni huduma.


Kwa upande wake ofisa Tawala Mkuu kutoka Wizara ya Maji,Jacob Kingazi akisoma mapendekezo ya kamati iliyoundwa na Waziri Aweso kwaajili ya kufanya tathimini ya hali ya upatikanaj wa huduma ya maji mji wa Karatu,alisema lazima kuwepo Kwa chombo kimoja kitakachosimamia utoaji wa huduma katika mji wa karatu ili kuondoa migogoro.

Kingazi alisema awali walibaini bodi kuendelea kutekeleza baadhi ya majukumu ya kiutendaji ilhali ilifikia ukomo mwaka 2019 ikiwemo ukusanyaji wa ukusanyaji mapato.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Karatu Dadi Kolimba,alimshukuru Waziri Aweso kwa kutoa maagizo hayo kwani wananchi watanufaika na bei moja badala ya awali kuwa na mkanganyiko wa bei kati ya Karuwasa na Kaviwasu

Alisema baada ya Rais Samia kutangaza filamu ya Royal Tour watalii wamefurika wilayani Karatu na hivi sasa hoteli zaidi ya 60 zilizopo hapo zinahitaji maji hivyo aliomba wilaya hiyo kupewa zaidi vipaumbele vya maji ili kuwezesha kila mtu kunufaika na huduma za maji.

Aidha alimshukuru Rais Samia Kwa kutoa kiasi cha shilingi bilioni 4.5 za mradi wa maji wilayani humo kwani itasaidia kabisa kumaliza tatizo la maji wilayani hapo ambapo alisema kuwa mita za ujazo 8254 zinaitajika ,jumla ya mita za ujazo 6980 zinapatikana na kunaupungufu wa Lita za ujazo 1274.

Kwa upande wake diwani kata ya Qurus Danstan Panga akitoa maoni katika kikao kazi hicho alimshukuru Waziri,Aweso kwa kuunganisha bodi hizo mbili na kuwa moja kwaajili ya kuleta maendeleo kwa wananchi na kuongeza kuwa hivi sasa watafanya vikao kwa wanachi kwaajili ya kuwaeleza wananchi kulipa ya bei hiyo ya unit 1,300 kwa kila mmoja badala ya sh,2000 hadi 3000 zinazotozwa na Kaviwasu .

 

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates