BREAKING NEWS

Tuesday, August 9, 2022

TMDA YAITAKA JAMII KUWA MAKINI PINDI WANAPO NUNUA DAWA

 

Wa pili kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kaskazini TMDA Proches Patrick,akiwa pamoja na wafanyakazi kutoka Mamlaka hiyo wakifurahia kombe mara baada ya ushindi wa pili wa Taasisi za Usimamizi na Udhibiti nanenane 2022


Mmoja wa Mtumishi wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba akiendelea kutoa elimu katika Maonyesho ya Nanenane katika viwanja vya Themi Njiro Mkoani Arusha 2022


Dawa ambayo inajulikana kwa jina la 60 minutes- Male Genital Desensinsitizer Spray (The Delay Spray for men)iliyokamatwa na Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba katika mpaka wa Namanga.


Dawa inajulikana kwa jina la Increase MK II (Men’s Penis enlargement) kuongeza maumbile kwa wanaume,iliyokamatwa katika mpaka wa Namanga .

Mamlaka ya Vifaa Tiba (TMDA) kanda ya kaskazini imeitaka jamii kuwa makini wakati wanaponunua dawa na kuwataka kuzichunguza vizuri kabla ya kuzitumia na kama watakuwa na mashaka juu ya dawa hizo, watoe taarifa kwa Mamlaka hiyo ili hatua za haraka za kisheria zichukuliwe

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkuu wa kanda ya kaskazini TMDA Proches Patrick wakati akiongea na waandishi wa habari katika  maonyesho ya sikukuu ya wakulima na wafugaji (nane nane) yanayofanyika katika viwanja vya Themi jijini Arusha ambapo alisema  dawa bandia ni tatizo kubwa  kwani wapo waingizaji na wasambazaji ambao siyo waaminifu ,wanaojali maslahi yao kuliko Afya za walaji, jambo ambalo husababisha madhara kwa binadamu,na kupunguza uaminifu kwenye mfumo mzima wa utoaji huduma ya Afya.

Aidha  aliainisha baadhi ya dawa zilizokamatwa na mamlaka hiyo,ambazo hazijasajiliwa ni pamoja na 60 minutes- Male Genital Desensinsitizer Spray (The Delay Spray for men) inayosababisha kuchelewa kufika kileleni kwa mwanaume,Increase MK II Men’s Penis enlargement) kuongeza maumbile kwa wanaume

‘’Dawa hizi tumezikamata hazijasajiliwa na wala hazina vibali vya usambazaji na uuzaji wa dawa hizo nchini,na wala sisi kama TMDA hatujaitathimini na kusajili dawa hizi kabla ya kuruhusiwa kuingia sokoni maana sisis tunasimamia ubora usalama na ufanisi wa dawa vifaa tiba na vitendanishi "Alisema Proches

Adha alisema kuwa lengo kuu la Mamlaka hiyo kushiriki katika maonyesho ya sikukuu ya wakulima na wafugaji  ni kutoa elimu kwa wananchi kwani afya yao ndiyo mtaji wao hivyo wakiwa salama wataweza kufanya shughuli za uzalishaji mali utakaopelea  uchumi wa nchi  kukuwa vyema

Aliwataka wananchi kutambua kuwa kutumia bidhaa ambazo hazijasajiliwa ni hatari kwa afya zao,maana hawajui mtengenezaji alikuwa anakusudia kutengeneza kitu gani ,hivyo jukumu kubwa ni kuhakisha kwamba vitu ambacho wanavitumia ni kile ambacho mamlaka hiyo imethibitisha.

‘’Mamlaka inaendelea kuwakamata wale wote wanaovunja sheria na kuwafikisha mahali panapowastahili, wananchi nunueni bidhaa kwenye maduka yaliyosajiliwa na TMDA pamoja na tasisi za Serikali ,msinunue kwenye vyombo vya usafiri,wala wale wanaopitisha bidhaa mkononi ,nunueni sehemu ambayo mtapewa risiti halali’’Alisisitiza

maonyesho haya yamebebwa na  kauli Mbiu isemayo ajenda 10/30 Kilimo ni Biashara Shiriki Kuhesabuiwa kwa Mipango Bora ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates