Na Woinde Shizza , ARUSHA
Taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo nchini (TEMDO) imebuni mtambo mpya wa kisasa wa kusafisha mafuta ya alizeti kwa kiwango cha juu kwa ajili ya matumizi salama ya binadamu.
Taasisi hiyo imeutambulisha mtambo huo kwa mara ya kwanza Kwa mikoa ya Kanda ya kaskazini katika maonyesho ya 28 ya sikukuu za wakulima nchini (Nane Nane) yanayoendelea katika viwanja vya Themi Njiro ndani ya halmashauri ya jiji Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko katika taasisi hiyo,dkt Sigisbert Mmasi alisema katika maonyesho haya ya nane nane wameweza kuleta teknolojia nne ambazo hawajawahi kuzileta katika maonyesho hayo ambazo ni mtambo wa kuchakata mafuta ya alizeti ambao unaanzia kwenye mashine ya kupokea mbegu unafata mashine ya kukamua mafuta,ukisha kamua unaenda kwenye mashine ya kuchuja ukisha maliza kuchuja ndio unaenda kwenye mtambo Kwa ajili ya kusafisha mafuta hayo.
" Unajua ukiangalia mafuta mengi yanayouzwa uko mtaani unakuta yamekamuliwa na mkulima na kuchujwa na kuuzwa apo apo na muda mungine unakuta mtu anasifia mafuta hayo kwakuwa ameona yanavyo kamuliwa lakini mafuta yale yanakuta sio mazuri bila ya kusafisha kwasababu yanakuwa bado nimafuta ghafi,nikisema ghafi ni mafuta ambayo ndani yake yana kitu kama gundi ,uchafu pamoja na vitu vingine ambavyo vina athari Kwa afya ya binadamu"alisema Mmasi
Alisema kwamba mtambo huo utasaidia kusafisha mafuta ghafi ya alizeti ambayo yana athari kwa afya ya binadamu na kuyasafisha katika ubora unaoitajika huku akiwataka wakulima kuwekeza katika mtambo huo kwa manufaa ya biashara zao na afya ya mlaji
Sambamba na mtambo huo mitambo mingine iliyobumiwa na taasisi hiyo ni ,mtambo wa kuchakata Sukari,mtambo wa kukamua mafuta ya Parachichi, vifaa tiba ambavyo Kiteketezi taka hatarishi za hospitali za hospitali , Vitanda vya kujifungulia wa Mama Wajawazito, Vitanda vya kukagulia na Kulazia Wagonjwa,stand ya drip , jokofu la kuhifadhia maiti pamoja kabati la kuifadhia vitu vya mgonjwa ambapo alibainisha kuwa Kwa sasa TEMDO inavifaa Tiba vyenye ithibati zaidi ya kumi na tano (15) vyenye ithibati ya TMDA.
Alisema lengo kuu la kutengeneza Vifaa Tiba ni pamoja na kuweza kusaidia kupunguza matumizi ya fedha za kigeni kuagiza nje ya nchi, kuongeza ajira za ndani na kurahisisha upatikaniji wa bidhaa kirahisi na kwa bei nafuu
Akiongelea mtambo wa kuchakata sukari alisema kuwa mtambo huu utasaidia sana kuongeza ajira Kwa watanzania pia itasaidia kupunguza tatizo la masoko Kwa wakulima wa miwa kwani Kiwanda kitakuwa na uwezo wa kuchakata Tani 20 za Sukari kwa Siku ambazo ni sawasawa na Tani 200 miwa
Awali akiongea katika maonyesho hayo mkuu wa wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango alizitaka taasisi za kilimo kubuni zana mbalimbali zitakazowasaidia wakulima katika shughuli zao ambapo aliipongeza taaisisi ya Temdo kwa ubunifu wa mitambo mbalimbali itakayosaidia maendeleo ya kilimo, mifugo na uvuvi nchini .
Alifafanua kuwa, maonyesho hayo yanatarajiwa kuchangia ukuaji wa mabadiliko kwa wakulima kutoka maeneo mbalimbali endapo elimu ya kutosha itatolewa na kuenea kwa kwa jamii inayowazunguka juu ya kilimo na ufugaji wa kisasa ambapo pia aliwataka watalaamu wa kilimo nchini kuendelea kutoa elimu ya kutosha kwa wakulima na wafugaji ili walime na kufuga kisasa na kuepukana na kuondokana na zana za zamani na hatimaye kuweza kubadilisha maisha yao.
Naye Mkuu wa wilaya ya Kiteto ,Mbaraka Alhaji Yusuph alisema kuwa,maonyesho hayo yameshirikisha waonyeshaji 200 kutoka Taasisi mbalimbali licha ya taarifa kuchelewa juu ya uwepo wa maonyesho,lakini mwitikio bado ni mkubwa sana.
Alitaja kaulimbiu ya maonyesho hayo Kwa mwaka huu kuwa ni "kilimo ni biashara ,shiriki kuhesabiwa Kwa mpango bora ya kilimo ,mifugo na uvuvi"ambapo aliwasiitiza wananchi Kushiriki katika zoezi la sensa .
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia