BREAKING NEWS

Tuesday, August 9, 2022

CAMARTEC YAJA NA SULUISHO LA MALISHO YA MIFUGO KATIKA KIPINDI HICHI CHA MABADILIKO YA TABIA NCHI



Fundi mchundo kutoka kituo cha zana za kilimo na teknolojia vijijini (CAMARTEC) Jeremia Simoni akiwaonyesha wakulima waliouthuria katika Banda lao lililopo katika maonyesho ya 28 ya wakulima na wafugaji nanenane yanayofanyika katika viwanja vya themi njiro mkoani Arusha Kwa upande wa mikoa ya Kanda ya kaskazini juzi jinsi mashine ya kufunga majani ya malisho inavyofanya kazi   



 Kutokana na tatizo la ukosefu  wa malisho  ya mifugo katika mikoa ya  Kanda ya kaskazini ikiwemo Arusha ,Manyara ,Tanga na Kilimanjaro linalosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi ,kituo cha zana za kilimo na teknolojia vijijini (CAMARTEC) kimemletea mkulima suluhisho Kwa kumtengezea mashine itakayomsaidia kukata, kufunga  majani  Kwa ajili ya kuhifadhi malisho yatakayo msaidia  katika kipindi ambacho hakuna mvua na malisho hayapatikani.


Akiongea na waandishi wa habari katika maonyesho ya 28  ya wakulima yanayoendelea kufanyika katika viwanja vya nane nane themi Njiro mkoani hapa ofisa uenezi na mafunzo kutoka CAMARTEC  Peter Mtoba alisema kuwa katika msimu huu wameamua kuwaletea wafugaji teknolojia hizo ili kuweza kupunguza tatizo kubwa linalowakabili wananchi la  chakula cha mifugo.

Alisema kuwa tatizo hilo limetokana na ukosefu wa mvua Kwa kipindi cha mda mrefu huku akitolea mfano katika mwaka huu mvua za masika ziliweza kumalizika katika kipindi cha miezi mitatu iliopita hali iliyopelekea mazao mashambani kuathirika Kwa kiasi kikubwa  na  wakulima kutopata chochote na kupelekea kile ambacho mfugaji alikuwa  anategemea kukipata baada ya mavuno kutopatikana tena kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo asilinia kubwa ya mazao mashambani yameathiriwa na baridi.

Alibainisha kuwa Kwa kipindi cha mwaka huu inategemewa kwamba tatizo la chakula cha mifugo kitakuwa na changamoto kubwa ambayo inaweza ikapelekea mifugo mingi kupoteza maisha .

"Kupitia mashine hiI ambazo tumeweza kuwaletea wakulima na wafugaji wanaweza kufaidika katika njia mbalimbali Kwa mfano yale mabua ambayo wakulima walikuwa wakiyapata kutokana na mavuno walikuwa wakisafirisha Kwa gharama kubwa sana Kwa mfano mfugaji akikodi kenta Moja ambayo inaweza kubeba tani nne anaweza kusafirisha majani kidogo sana kwagharama ya kiasi cha shilingi laki tatu ,lakini pia akifikisha yale majani sio yote yatalika  na mifugo  kutokana na kuharibika  kiasi ambacho zaidi ya asilimia 90% ya yale mabua ng'ombe hayali yakifika katika eneo la kuhifadhia ,iwapo atatumia mashine hizo anaweza akakata kata mazao na kuyafunga na akasafirisha magunia mengi yaliyofugwa kutokana na uwezo wa gari "alibainisha Peter

Alisema kupitia teknolojia hizo  zitamsaidia mkulima kuokoa chakula cha mifugo Kwa zaidi ya asilimia 90% ,pia zitamsaidia mfugaji kuhifadhi chakula kingi cha mifugo katika eneo dogo kitakacho muwezesha kuilisha mifugo yake katika kipindi chote ambacho kitakuwa na tatizo la chakula cha mifugo.

Aidha aliwataka wakulima  nchini wametakiwa kubadilika na kuachana na ufugaji wa mazoea bali wafuge kisasa kwa ajili ya kupata mazao mengi lakini yenye ubora ambayo yataweza kuuzika kwa faida na hivyo kuongeza mchango wa pato la Taifa.

 Alisema ufugaji wa kisasa unaleta manufaa makubwa hata ukiwa na mifugo michache ambayo utaitunza vizuri tofauti na kuwa na idadi kubwa ya mifugo ambayo hawasaidii kuinuka kiuchumi ambayo pia itakufanya ushidwe kuilisha kutokana na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi 

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates