BREAKING NEWS

Wednesday, August 10, 2022

FIFA YAHAIDI KUISAIDIA TANZANIA


Rais wa Shirikisho la Soka Duniani(FIFA) Gianni Infantino  amesema  FIFA itaendelea kuisaidia Tanzania kutokana na kuridhishwa na jitihada
mbalimbali zinazofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Michezo.
 

Akizungumza usiku wa kuamkia leo Agosti 10, 2022 mara baada ya kupokelewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Mohamed Mchengerwa katika kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro amesisitiza kuwa FIFA itaendelea kuisaidia Tanzania. 

Akiongozana na wachezaji mahiri wa zamani waliopata kucheza katika makombe ya dunia na mwamuzi  Corina amesema amefurahishwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tanzania. 



“Tayari FIFA imekwishatoa msaada wa ujenzi wa viwanja changamani Dar na Tanga lakini wako tayari kwa ajili ya kuongeza vituo katika kanda nyingine” amefafanua  Mchengerwa 

Aidha Mchengerwa amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa kwenye michezo ambayo imesaidia Tanzania kupiga hatua duniani katika. 

Mchengerwa amepokea viongozi mbalimbali wa juu kwenye mashirikisho ya Soka duniani na kufanya  vikao vya kuendeleza michezo ambao leo wanahudhuria mkutano Mkuu wa 44 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) jijini Arusha. 

Aidha  Mchengerwa ametumia fursa hiyo kuahidi kuendelea kuimarisha mahusiano na nchi mbalimbali ambazo tayari ziliahidi kuendeleza mashirikiano katika sekta za michezo, Sanaa na Utamaduni.

Mkutano.




Aidha mkutano huu wa  kihistoria umehudhuriwa na zaidi ya watu mia tano na waandishi wa habari zaidi ya mia moja huku ukiangaliwa na
zaidi ya watu bilioni moja.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates