BREAKING NEWS

Wednesday, August 3, 2022

WAUZAJI NA WASAMBAZAJI WA MBEGU WATAKIWA KUENDELEA KUTOA ELIMU YAKUTOSHA KWA WAKULIMA


Mkuu wa wilaya ya Arumeru,Muhandisi Richard Ruyango amewataka wauzaji na wasambazaji wa mbegu(Kibo Seed)kuendelea kutoa elimu kwa wakulima kuanzia ngazi ya chini ili kuweza kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali nchini.






Akizungumza baada ya kutembelea banda la maonyesho ya Kibo seed katika viwanja vya nane nane ambayo kanda ya kaskazini yanafanyikia jijini Arusha,Muhandisi Ruyango alisema ameridhishwa na uzalishaji wa kampuni hiyo kwani kwa kuwapa elimu wakulima wengi kutasaidia kuongeza tija zaidi katika sekta hiyo.






"Kweli nimeridhishwa na uzalishaji wenu lakini ni vyema elimu hii ikawafikia wakulima ili kuweza kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao mbalimbali kutokana na Teknolojia zenu muhimu,"alisema Muhandisi Ruyango.






Naye Afisa Masoko wa Kampuni ya Kibo Seed,Franco Frederick alisema anashukuru ujio huo wa Mkuu huyo wa wilaya kwani umekuwa chachu katika kuhakikisha wanawafikia wakulima wengi zaidi ili waweze kupata elimu hiyo ya Teknolojia ya uzalishaji wa mazao mengi hususani Mahindi.






"Kitu kikubwa alichotusihi sisi kuona elimu hii inawafikia wakulima wengi zaidi nchini hivyo tumepokea ushauri huo katika kuhakikisha usambazaji wa mbegu unawafikia kwani utofauti wetu umeonekana kati ya mashamba ya wananchi," alisema Afisa huyo.






Alisema bidhaa zao zimekuwa na utofauti na kuleta tija kwa wakulima kutokana na wanaenda na wakatika katika kuboresha pembejeo ili uzalishaji wa mazao uongezeke hasa matumizi ya mbegu chotara.






Aidha aliongeza kuwa kwa upande wa mbogamboga na nafaka huwa ni chotara zinazozaa kwa wingi na kumsaidia mkulima kutoka kwenyw kilimo cha kujikimu na kuingia kwenye kilimo biashara ambapo atapata mazao mengi zaidi.







Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates