Mbunge
wa Viti maalum Mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose
Tweve akiongea na vijana wa UVCCM kwenye moja ya baraza alilohudhuria
Mbunge
wa Viti maalum Mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose
Tweve akiwa na furaha na vijana wa UVCCM mkoa wa Iringa alipokuwa mgeni
rasmi kwenye moja ya mabaraza ya vijana hao.
Mbunge
wa Viti maalum Mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose
Tweve akiwa na mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Iringa Vijijini.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mbunge wa Viti maalum Mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Rose Tweve ameipongeza jumuiya ya Umoja Wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kukijenga chama.
Mbunge
Rose Tweve alisema kuwa vijana wamekuwa wanafanya kazi kubwa wakati wa
uchaguzi na kwenye kampeni mbalimbali za serikali kama ambavyo hivi Sasa
wanavyofanya kwenye SENSA.
Alisema
kuwa ni muhimu Kwa Kila mwananchi kuhesabiwa katika zoezi Hilo la sensa
Ili kuiwezesha Serikali kupanga bajeti Kwa usahihi Ili kufikisha
maendeleo Kwa Kila mwananchi kulingana uhitaji na idadi kamili ya watu.
Katika
hatua nyingine mbunge Rose Tweve alisema kuwa bajeti ya mwaka 2021/2022
imesheheni miradi mingi ya kimaendeleo kama vile
barabara,elimu,afya,Kilimo na ni bajeti ambayo itasaidia kutatua
changamoto za wananchi wote.
Tweve
aliwaomba vijana kuendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya
kuleta maendeleo katika kila sekta hapa nchini jambo ambalo linawafanya
wananchi kukuza uchumi wao na taifa kwa ujumla.
Alimazia
kwa kusema kuwa hiki ni kipindi cha uchaguzi hivyo vijana wanapaswa
kugombea nafasi mbalimbali na kushiriki katika jumuiya mbalimbali ambazo
zinaendelea kufanya uchaguzi ili kupata viongozi walio bora kukiongoza
chama cha mapinduzi (CCM).
Mbunge
huyo alifanikiwa kutembelea mabaraza yote ya umoja wa vijana wa chama
cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa ambayo ni Baraza la UVCCM Iringa
vijijini, Manispaa ya Iringa, Mufindi na kilolo.
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia