BREAKING NEWS

Saturday, July 30, 2022

TOENI KWA VIONGOZI WA DINI ILI WAWEZE KUZIFIKIA JAMII ZA PEMBEZONI KUWAKUZA KIROHO :SHEIKH SHAABAN

 Na Ahmed Mahmoud


SHEIKH wa Mkoa wa Arusha Shabaan Jumaa bin Abdallah Amewataka waumini wa Dini ya kiislam kujenga mazoea ya kujitolea kwa viongozi wa Dini na wahitaji wengine ili waweze kufanyakazi ya Daawa kila eneo.

Sheikh Shabaan Ameyasema hayo wakati akipokea msaada wa Gari uliotolewa na Taasisi ya Sheikh Shariff Foundation katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika Jijini Arusha.

Alisema kwamba wapo viongozi wengi wanapata ugumu wa kufikisha ujumbe kwa jamii za pembezoni na kuwataka wafadhili wengine pamoja na hao kuona Wakati huu kuwaangalia nao sanjari na kutengeneza Taasisi ziweze kusimama.

"Niwaombe sana Mimi nimekuwa napata taabu sana kipindi Cha nyuma kwenda kulingania maeneo ya pembezo mwa Mjini ila Mjini ni rahisi kufikika ambayo sikuweza kufika Kutokana na adha ya usafiri ila Sasa baada ya kupata Gari hili na la kwanza ambalo lilitolewa na Leopard Tour nashukuru Alhamdulilah ila Mimi sio Kiongozi pekee muwaangalie na viongozi wengine Ishaallah"

Akizungumzia Taasisi ya Sheikh Shariff amesema imefanya mengi makubwa katika mikao ya Kigoma Tabora Singida na kuacha alama kubwa kwa uislamu katika maeneo hayo kwani wanapofanya Da'awa kile wanachopata huwaachia waislam wa eneo hilo hapa kwetu wametoa fedha kwa kinamama misikiti na hata ofisi ya Sheikh wa mkoa.

Awali akiongea katika hafla hiyo Sheikh Shariff Mikidadi Matongo ameahidi kwamba atatoa zaidi ya TSH 3 million kuweza kuendeleza uislamu ikiwemo ukarabati wa ofisi ya Bakwata Wilaya sanjari na ukarabati wa vyoo vya msikiti Mkuu wa Arusha.

Akiongelea Gari aliotoa kwa Sheikh wa mkoa amesema kwamba hii ilitokana na kuona waislamu hawana Utamaduni wala mwamko wa kutoa Alhali wanavyo hivyo kuonyesha faida ya kuwatunuku na kuwathamini viongozi wetu na hata dini yetu ili kuweza kwenda Mbele

"Siku moja nilikuwa na muhadhara hapa Mjini nikamuita Sheikh miye nilitangulia pale nilipouliza Sheikh yupo wapi mara namuona anakuja na bajaji hii ilinistua sana na kunihuzunisha ingawa Taasisi yetu haina fedha nilimuomba Allah anwafikishe ili ninunue Gari hili na Ishaallah nimetimiza hilo" 

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates