BREAKING NEWS

Wednesday, July 13, 2022

KATIBU WA CCM WILAYA YA MBINGA AWATAKA VIJANA KUTHAMINI MICHANGO YA VIONGOZI WA CCM.

 


 



Na Amon Mtega,_Mbinga


KATIBU wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma Jacob Siayi amewataka Vijana wa Wilaya hiyo kuendelea kuthamini michango ya kazi  zinazofanywa na Viongozi wa Chama hicho ili wazidi kusongambele kimaendeleo zaidi.


Wito ameutoa wakati akikabidhi jezi za kuchezea mpira wa miguu  zenye  thamani zaidi  sh.160,000 pamoja na mpira wa miguu kwenye timu ya vijana wa kikundi cha Riverside Daks kilichopo kwenye tawi la CCM la Ngamanga kata ya Matarawe Wilaya ya Mbinga.


Siayi ambaye amealikwa kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano mfupi wa akikabidhi jezi hizo zilizonunuliwa na mwenyekiti wa tawi la CCM la Ngamanga Hilmara Ndunguru amesema kama vijana watawatumia vema Viongozi wa Chama hicho waliyopo kwenye maeneo yao baadhi ya changamoto zitapungua na kuwafanya wasongembele kimaendeleo.


Katibu huyo licha ya kukabidhi jezi hizo pia amekabidhi  trubai lenye dhamani ya zaidi sh.20,000,kwenye kikundi cha Lulambo mnalani ambacho nacho ni cha Vijana huku akimpongeza mwenyekiti wa tawi hilo Hilmara Ndunguru kwa kuwajali Vijana hao .


Hata hivyo amewataka baadhi ya Viongozi wa kwenye chama CCM pindi wanapokuwa wamechaguliwa wafanye kazi na jamii begakwabega kama alivyoonyesha mfano mwenyekiti wa tawi la Ngamanga pamoja na Viongozi wengine ambao nao wamekuwa wakijitahidi kuwa na jamii .


 Aidha katibu huyo ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha Vijana kuwa wajiandae na suala la sensa mwaka huu ili bajeti ya Serikali iendane sawasawa na idadi ya watu wake huku akiwataka Vijana hao pia kutambua kazi kubwa inayofanywa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kutuletea maendeleo.



Kwa upande wake mwenyekiti wa tawi hilo Hilmara Ndunguru amesema kuwa ameamua kutoa msaada huo kwa Vijana baada ya kutambua kuwa wanatimu lakini inachangamoto za jezi za kuchezea jambo ambalo lilikuwa likiwakatisha tamaa kwenda kucheza mashindano na timu zingine.


Mwenyekiti huyo akizungumzia msaada wa trubai amesema kuwa kikundi hicho ni cha waendesha boda hivyo trubai litawasaidia kujikinga na jua pamoja na mvua pindi wanapowasubiri wateja wao.


Nao Vijana waliyopatiwa msaada huo wamekipongeza Chama cha Mapinduzi CCM kupitia Viongozi wake kwa kuwajali Vijana  jambo ambalo wamedai kuwa linawafanya waendelee kufanya kazi kwa bidii.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates