BREAKING NEWS

Wednesday, July 13, 2022

WIZARA YA MADINI YASHUSHA NEEMA KWA WACHIMBAJI WADOGO.

 


WAZIRI wa Madini Dkt.Doto Biteko,akizungumza na wandishi wa Habari Mkoani Geita kuhusu  utekelezaji wa vipaumbele vya Bajeti ya wizara ya madini kwa mwaka wa fedha 2022/2023.

…………………………

Na. Costantine James, Geita.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia wizara ya Madini Imepanga kuwaendeleza wachimbaji wadogo wa Madini hapa nchini kwa kuwatengea maeneo pamoja na kuwapatia Leseni za uchimbaji kwenye maeneo ambayo yana taarifa za Msingi za Kijiolojia.

Hayo yasemwa na Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko wakati akizungumza na wandishi wa Habari Mkoani Geita amesema katika utekelezaji wa vipaumbele vya Bajeti ya wizara yamadini kwa mwaka wa fedha 2022/2023 Wizara imejipanga kuwaendeleza wachimbaji wadogo kwa kuwawezesha kuwa wakati na hatimaye kuwa wakubwa.

Dkt. Biteko amesema katika mwaka wa fedha 2022/2023 serikali imelenga kuwasadia zaidi wachaimbaji wadogo kwa kutoa leseni pamoja na huduma ya utafiti kwa gharama nafuu ili kuwawezesha wachimbaji wadogo kufanya kazi zao kwa urahisi zaidi ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Waziri Dkt. Biteko amese ili kuwawezesha wachimbaji wadogo kuwa wakubwa wizara imejipanga kuwapa mafunzo wachimbaji wadogo yanayohitajika kuhusu uchimbaji, uchenjuaji pamoja na Biashara ya madini kwa lengo la kukuza sekta ya madini hapa nchini.

Amesema mchango wa wachimbaji wadogo wa madini umeongezeka kutoka asilimia 44% kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ukilinganisha na asilimia 30% ya Mwaka wa fedha 2020/2021.

Waziri Biteko amesema sekta ya Madini kwenye pato la taifa umeimarika ambapo katika kipindi cha Januari hadi Septemba 2021, uliongezeka hadi kufikia wastani wa asilimia 7.3% kutoka wastani wa asilimia 6.5 katika kipindi kama hicho 2020.

Waziri Biteko amesema wizara ya madini katika mwaka wa fedha 2022/2023 imejipanga kukusanya jumla ya shilingi bilioni 894.3 kiasi ambachoo ni ongezeko la asilimia 22.12% ikilinganishwa na bilioni 696.4 zilizopangwa kwa mwaka wa fedha uliopita 2021/2022.

Kwa upande wake Gabriel Masanyiwa Msimamizi wa Kituo cha mfano cha uchenjuaji wa Dhahabu Katente Bukombe Geita wakati akisoma taarifa fupi ya kituo hicho mbele ya Waziri wa madini amesema kituo hicho tangu kuanzishwa 2020 kimewezesha kuzalisha dhahabu katika CIP na Elution yenye thamani ya bilioni 5.3.

Mpaka sasa kituo hicho cha mfano cha uchenjuaji wa madini ya dhahabu Katente Bukombe Geita kituo kimefanikiwa kuliingizia mapato shirika la madini la Taifa STAMICO kiasi cha milioni 420,331,899.52 kutokana na kutoa huduma ya uchenjiaji wa mbale wa dhahabu katika mtambo wa CIP na Elution kwa wachimbaji wadogo.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates