BREAKING NEWS

Thursday, July 7, 2022

MENEJA WA KIWANJA CHA NDEGE ARUSHA ALEZEA SWALA LA NDEGE KUUNGUA MOTO KATIKA ENEO HILO

 



Meneja wa Kiwanja cha Ndege Arusha, Elipid Tesha amesema zoezi la ajali ya ndege kuungua moto katika eneo hilo limefanyika kwa lengo la kuona utayari wa Taasisi za uokoaji namna gani zinaweza kuwahi eneo la tukio na kila mmoja kuweza kutimiza wajibu wake.


Aidha, Elipid amesema zoezi hilo limegharimu zaidi ya Milioni 18 kuandaa na hufanyika kila baada ya miaka miwili.


"zoezi kama hili linagharimu kiasi kikubwa cha ela kwasababu kuna vikao, maandalizi ya vifaa na inachukua muda inaweza kuchukua hata miezi sita wakati wa kujiandaa" Elipid

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates